Tetesi zinasema, Manchester United inasaka mbadala wa kiungo wa England mwenye umri wa miaka 22 Declan Rice kufuatia dau kubwa la £80-90m wanalolitaka West Ham.
Antonio Rudiger anaweza kujizolea mshahara wa £400,000 kwa wiki kama ataikacha Chelsea, huku vilabu vya Bayern Munich na Juventus vikiwa tayari kumpa mshahara huo mnono mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 28 kutoka ule wa £130,000 kwa wiki anaolipwa.

Borussia Dortmund wanamfuatilia mshambuliaji wa Manchester United mfaransa Anthony Martial, 25, kama mbadala wa mshambuliaji wake raia wa Norway Erling Braut Haaland, 21.
Tetesi zinasema, Manchester City wanataka kuipiku Real Madrid katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Paris St-Germain mfaransa Kylian Mbappe, 22 msimu ujao.
Tetesi zinasema, Real Madrid ilikataa ofa ya Arsenal ya £34m ya kumsajili kiungo wake raia wa Hispania Marco Asensio,25, msimu huu.
Tetesi zinasema, Atletico Madrid wanamtaka mshambuliaji wa Arsenal na England mwenye umri wa miaka 22 Bukayo Saka.

Chelsea itaachana pia na mpango wake wa kumuwania mlinzi wa kifaransa kutoka Sevilla Jules Kounde, 22, na mlinzi wa kati wa PSG mbrazil Marquinhos, 27, ili kuelekeza nguvu zake za kumsajili mlinzi wa Juventus na Uholanzi mwenye umri wa miaka 22 Matthijs de Ligt.
Tetesi zinasema, Juventus wanaendelea na mazugumzo na mshambuliaji raia wa Argentina Paolo Dybala, 27, kuhusu mkataba mpya ulioboreshwa zaidi.
Tetesi zinasema, Barcelona watamuuza kiungo wake mchezeshaji raia wa Brazil Philippe Coutinho, 29, katika dirisha la usajili la Januari.
Ni wakati wa ushindi mkubwa ukiwa na kasino bomba ya Lock a Luck, meridianbet wanakupa sababu ya ushindi, funga bahati yako ya ushindi ukiwa na mabingwa.



Sania+mapua
Tetesi za kweli kabisa