Paris Saint-Germain inajiandaa kumenyana na mabingwa watetezi wa Ligue 1, Lille bila Kylian Mbappe, baada ya fowadi huyo wa Ufaransa kuondolewa rasmi kutokana na maambukizi ya sikio, pua na koo (ENT).

Mbappe anaendelea na matibabu ya ugonjwa huo kwa sasa na kurejea kwake mazoezini hakupangwa hadi Jumatatu, kama ilivyowekwa wazi katika taarifa iliyotolewa na idara ya matibabu ya PSG.
“Kylian Mbappe bado anaendelea na matibabu ya ugonjwa wake wa ENT na ataanza mazoezi mwanzoni mwa wiki ijayo,” taarifa hiyo ilisoma.
Maambukizi haya sio tu kwamba yanamweka Mbappe nje ya Mechi ya nyumbani dhidi ya Lille, lakini kuna uwezekano kwamba hatajumuishwa kwenye kikosi cha mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya RB Leipzig ambayo itafuata.
Wakati huohuo kocha wa PSG Mauricio Pochettino hajaweka wazi kama Lionel Messi atacheza mchezo huo kutokana na mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina kuwa na tatizo dogo la misuli.
Mchongo wa mkwanja mrefu kutoka kasino bora za mtandaoni za Meridianbet. Mchezo wa Circus Fever unakuweka katika nafasi nzuri ya kuwa mshindi. Furahia kasino maridhawa kutoka nyumba ya mabingwa meridianbettz.

CHEZA HAPA

