Kocha mkuu wa muda wa klabu ya Manchester United Ralf Rangnick anajiandaa kumuongeza Chris Armas kwenye benchi lake la ukufunzi huko Manchester United.

Kocha huyo raia wa Ujerumani anaangazia kuimarisha timu yake ya ukocha kwa kuongeza wakufunzi kadhaa lakini vizuizi vya kupata visa imefanya mchakato uwe mgumu.
Armas ni Mmarekani mwenye umri wa miaka 49 aliwahi kufanya kazi katika MLS ambapo alichezea LA Galaxy na Chicago Fire, na timu ya yaifa ya USA.
Alisimamia New York Red Bulls kati ya 2018-2020, ambapo alifahamiana na Rangnick. Rangnick alipandishwa cheo mwaka 2019 kuwa mkuu wa michezo na maendeleo kwa franchise ya Red Bull, ambayo ilijumuisha klabu ya New York.
“Nina furaha zaidi kufanya kazi na wakufunzi wa sasa kwa sababu nahitaji uzoefu wao, nahitaji ujuzi wao kuhusu kikosi cha sasa,” alisema. “Ni wazi nitajaribu kutafuta mtu mmoja, wawili, au watatu ambao wanaweza kujiunga nasi katika wiki moja au mbili lakini kutokana na kanuni za Brexit sio rahisi sana.
Unaweza kujishindia mamilioni katika kasino yako pendwa ya meridianbettz, mchezo wa Agent Jane Blonde Return ni moja ya michezo inayopendwa kwasasa huku ikiwafanya wachezaji kuwa mamilionea kila siku. Unasubiri nini! ungana na Agent Jane Blonde akufanye milionea.
CHEZA HAPA


