Baada ya kusambaa taarifa za Manchester United kuweka mezani mkataba wa ofa mpya kwa Paul Pogba, kiuhalisia, mambo hayapo hivyo!
Pogba anamaliza mkataba wake wa miaka 5 na Man United ifikapo Juni 30, 2022. Hata hivyo, hakuna ofa yeyote mpya aliyopewa mchezaji huyo toka ile aliyopewa mwishoni mwa msimu uliopita.

Kwa hali ilivyo, Paul Pogba hakuikubali wala kuikataa ofa aliyopewa na The Red Devils na badala yake, anaendelea na maisha kama yanavyokwenda. Kinachoaminika ni kuwa, Pogba anazingatia zaidi kurejea kwake uwanjani (akitoka majeruhi) na kuendelea kuipambania Manchester United.
Japokuwa, Pogba anauwezo wa kusaini mkataba wa awali na klabu yeyote nje ya EPL kuanzia mwezi huu. Ila, hata hili halionekani likitokea na badala yake, Paul atasubiri mpaka mwishoni mwa msimu huu ndipo ataamua hatma yake – anabaki au anaondoka Old Trafford.
Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.


