Tetesi za Soka Barani Ulaya.

 

Tetesi zinasema, Manchester United wametoa ofa kwa kiungo wa kati Mfaransa Paul Pogba, 28,ya mkataba wenye thamani ya pauni 500,000 kwa wiki ili aendelee kubakia katika klabu hiyo.

Tetesi zinasema, Manchester United wanawinda saini ya kiungo wa kati wa Lazio na Serbia Sergej Milinkovic-Savic, 26.

Tetesi zinasema, mmiliki wa zamani wa Newcastle Mike Ashley anafikiria kuchukua dau la kuinunua klabu ya Derby County.

 

Tetesi zinasema, Liverpool wanajiandaa kutoa ofa ya mkataba kwa kiungo wa kati wa Barcelona na Uhispania Gavi, 17, wa malipo ya karibu pauni 80,000 kwa wiki ili kupata sahihi yake.

Everton wamepewa ofa ya mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na Manchester United wa Inter Milan Alexis Sanchez, 33, kwa uhamisho wa bila malipo.

Tetesi zinasema, Newcastle wameongeza dau lao kwa mlinzi wa Lille Sven Botman, 21.

Tetesi zinasema, Aston Villa wanavutiwa na kiungo wa kati wa Brighton wa Mali, Yves Bissouma, 25.

Mkufunzi wa Paris St-Germain Mauricio Pochettino yuko tayari kupokea ofa yoyote ya kuwa kocha wa Manchester United.

 

Pochettino

West Ham itakataa ofa yoyote ambayo Newcastle itampa mlinzi wa Ufaransa Issa Diop, 24.

Liverpool wamekataa dau la pauni milioni 7 kutoka kwa Watford kwa ajili ya mlinzi wa Uingereza Nathaniel Phillips, 24.

Sevilla hawako tayari kumruhusu mlinzi wa Brazil Diego Carlos, 28, ajiunge na Newcastle kwa chochote isipokuwa ada kubwa.

Kiungo wa kati wa Arsenal na Uingereza Ainsley Maitland-Niles, 24, amewasili Italia kabla ya kuhamia kwa mkopo katika klabu ya Serie A ya AS Roma.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.