Xavi Abaki Mdomo Wazi Mshahara wa Dembele

Kocha wa Barcelona Xavi inasemekana aliachwa mdomo wazi alipojua kwamba Ousmane Dembele anataka kandarasi ya pauni 700,000 kwa wiki kusalia Camp Nou.

Mkataba wa sasa wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa na wababe hao wa Catalonia unatarajiwa kufika tamati mwishoni mwa Juni, na Barcelona wanapata kigugumizi kukubaliana na matakwa ya mkataba wa mshambuliaji huyo.

Manchester United, Newcastle United na Liverpool wote wanaaminika kuwa na nia ya kumpeleka mshindi huyu wa Kombe la Dunia kwenye Ligi ya Premia kabla ya kampeni ya 2022-23.

XAVI and DEMBELE

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa Ujerumani Florian Plettenberg, madai ya mshahara wa Dembele ya pauni 700,000 kwa wiki yamemshtua Xavi, ambaye ameendelea kumuunga mkono Mfaransa huyo huku kukiwa na sintofahamu kuhusu mustakabali wake.

Mshambuliaji huyo yuko katika nafasi nzuri ya kudai mshahara mkubwa kutokana na hali ya mkataba wake, huku pia akiwa kwenye nafasi ya kupokea ada kubwa ya kusajiliwa kutoka kwa klabu mpya msimu huu wa joto.

Dembele, ambaye amejumuishwa kwenye kikosi cha mechi ya Jumapili ya La Liga dhidi ya Granada, amefunga mara moja na kutoa pasi mbili za mabao katika mechi tisa alizocheza katika ngazi ya klabu wakati wa kampeni za 2021-22.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe