Kocha mkuu wa Barcelona Xavi Hernandez anaendelea kupata wakati mgumu baada ya kushindwa kupata matokeo kwenye mchezo dhidi ya timu ya Granada wikendi iliyopita na amekuwa katika viulizo kwa baadhi ya maamuzi aliyofanya siku ya mchezo.

Swali kubwa linaloulizwa ni kwanini mchezaji Gavi aliendelea kuwepo uwanjani licha ya kinda huyo kuonyeshwa kadi ya manjano na mwishowe kuonyeshwa kadi ya pili na kutolewa na kuiweka timu kwenye wakati mgumu dakika za lala salama za mchezo.
Maamuzi mengine duni aliyofanya ni kumtoa Osamne Dembele ambaye alikuwa kwenye kiwango kizuri na kumuingiza mchezaji mchanga Alvaro Sanz na Xavi mwenyewe alikiri kufanya kosa kwenye jambo hilo wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
“Ni hatari ambayo tulichukua. Tulimhitaji Alvaro kwa sababu tulitaka kuwa na mpira,” alisema baada ya mchezo huo.
Uamuzi huo ulikuwa mgumu kuelewa ikizingatiwa kwamba Riqui Puig mwenye uzoefu zaidi aliachwa benchi.
Nyingine ilikuwa kuingizwa kwa Memphis Depay akimbadili Luuk de Jong, ambaye alikuwa mchezaji bora wa Barcelona usiku huo.
Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

CHEZA HAPA

