Mike Tyson na Ubaya Ulipozidi Wema

October 2 1980, Muhammad Alli anachakazwa vibaya sana na Larry Holmes. Kabla ya pambano madaktari walimkataza Alli kupanda ulingoni kutokana na hali mbaya ya afya yake. Ila walisahau huyu ni Muhammad Alli, binadamu asiyeamini katika kushindwa na kupoteza. Alilazimisha kupigana akiwa mgonjwa akaambulia kipigo cha ‘mbwa mwizi’

Jukwaani alikuwepo mshikaji wa karibu wa Alli, Cus D’Amato aliyekuja na mvulana mdogo wa miaka 14, Alimuokota katikati ya mji akiwanyang’anya watoto wa kizungu chakula na kuwapiga vibaya. Huyu mtoto aliiabudu mikono ya Muhammad Alli, Aliyahusudu maisha yake na kuuishi unyama wake. Huyu mtoto wa kuitwa Mike Tyson.

Mike Tyson alirudi nyumbani hawezi kuongea, hawezi kula wala kulala. Ilibidi Cus ampigie Alli simu na kumuambia “nipo na kijana fulani hapa, ana ndoto za kuwa Muhammad Alli, tafadhali ongea nae”. Tyson alishika simu na kuzungumza sentensi moja tu, “Jana nimekutazama ‘live’ kwa mara ya kwanza, usihofu nitakulipia kisasi siku moja.” Ikaisha hivo.

Muda haugandi na jua halikawii kuchwa, Larry Holmes alistaafu ngumi na kurudi nyumbani kupumzika. Tyson alikuja kuitikisa dunia. Holmes akiwa na miaka 38 alitamanishwa kurudi ulingoni kupambana na Tyson kwa kitita cha dola 3 milioni. Tyson alikuwa tayari kupambana bure, pesa si kitu mbele ya kisasi alichokifuga kwa zaidi ya miaka nane.

Pambano likaandaliwa na kupewa jina la ‘Heavy weight history’. Saa hiyo dunia inakumbuka kuwa Holmes hajawahi kupigwa kwa ‘KO’. Muhammad Alli alialikwa kama mgeni wa mpambano. Kabla ya kengele kulia alimfuata Tyson na kumnong’oneza “kumbuka ulichowahi kuniahidi, wakati ni sasa”. Tyson hakumuangusha, ndani ya raundi nne tu Holmes alikula KO ya kwanza ya maisha yake.

Historia yake inaanzia ndani ya jela ya watoto mjini New York akiwa na miaka 13. Hii ilikuwa mara ya 38 analetwa ndani kwa makosa tofauti. Maafande hapa walimshazoea, ilifika muda wakampa sero yake binafsi yenye jina lake. Alishazoea kuletwa hapa. Si Mapadre wa Roma wala Masheikh wa Saudia waliodhani kama Tyson anaweza kubadilisha tabia

ITAENDELEA..


Ondoka na Mkwanja Kwenye Tsh. 160,000,000

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu.

Soma Zaidi

28 Komentara

    Good news

    Jibu

    Duuh mohamedi Ali alikua gwiji

    Jibu

    Huyu ndo Mike Tyson

    Jibu

    Noma sana Tyson

    Jibu

    Mike tyson ngumi jiwe

    Jibu

    Tyson ni mwana ndondi mahiri sana

    Jibu

    tyson katika dimba la ngumi yupo makini sana na anahakikisha anapata ubingwa

    Jibu

    Goodupdate

    Jibu

    Tyson history yake haiwezi kufutika

    Jibu

    Nasubiria muendelezo jmn

    Jibu

    Huyo ndio Tyson alikuwa anaga kazi mbovu ana history nyingi yakimabavu

    Jibu

    Kumbe Muhammad ally ndiye aliyemtoa tyson

    Jibu

    Habari nzuri sana

    Jibu

    Habari nzuri

    Jibu

    Iron tyson alikua balaa na uwezo wake mkubwa ulimwengun

    Jibu

    Tyson ni mwana ndondi yuko vizur sana

    Jibu

    Habari njema sana

    Jibu

    Tayson yuko vizuri

    Jibu

    Tyson mnyama

    Jibu

    Iron tyson alikua balaa

    Jibu

    Saf

    Jibu

    Tyson Ni mwenye history ktk ulimwengu wa ndondi

    Jibu

    Mike TYSON ( iron MAN) mambo ni moto

    Jibu

    Mike Tyson MTU mbayaw

    Jibu

    duh nasubiria mwendelezo

    Jibu

    Tyson noma

    Jibu

    Noma sana Tyson

    Jibu

    Tyson mzee wa ngumi jiwe

    Jibu

Acha ujumbe