Joshua ana asili ya Nigeria na Wanigeria wanajivunia nyota huyo, kwani mama yake ni raia wa nchi hiyo. Pia, baba yake ana asili ya Nigeria na Ireland.
Kuthibitisha mapenzi yake kwa Afrika, bondia huyo amechora ‘tattoo’ ya ramani ya bara hilo kwenye mkono wake wa kulia. Alikulia Nigeria kabla ya kuhamia England alipokuwa na umri wa miaka saba.
Joshua alianza masumbwi mwaka 2007 akiwa na umri wa miaka 18. Aliyemvutia katika mchezo huo hatari ni binamu yake aitwaye Ben Ileyemi.

Miaka mitano baadaye, ndipo aliposhinda medali ya dhahabu katika michuano ya Olimpiki iliyofanyika jijini London, baada ya kumdunda aliyekuwa bingwa mtetezi, Roberto Cammarelle wa Italia.
Dawa za kulevya zilikaribia kumaliza maisha yake ya masumbwi na hiyo ilikuwa mwaka 2011. Alikutwa na dawa hizo aina ya cannabis, lakini alinusurika kifungo cha gerezani. Hata hivyo, alikumbana na hukumu ya kufanya kazi za jamii kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Anamkubali Barack Obama ile mbaya. Joshua amekuwa hafichi mapenzi yake kwa Rais Mstaafu huyo wa Marekani. Akihojiwa na kipindi kimoja cha televisheni, alisema anatamani siku moja angekaa meza moja na Obama.

Miaka mingi iliyopita, Klitschko aliwahi kumtabiria Joshua kuwa ndiye atakayekuja kutawala ulimwengu wa masumbwi na hicho ndicho kinachotokea sasa. “Hatima ya uzito wa juu wa mchezo wa ndondi iko chini ya Joshua.
“Sijawahi kuona bondia mkubwa, mwepesi na mwenye kipaji kama Anthony na kama ataendelea hivi, mchezo huo ni wake,” aliwahi kusema Klitschko.
Alipokuwa mdogo, Joshua alimpenda mwanamuziki 50 Cent, hasa albamu yake ya ‘Get Rich or Die Tryin’. Alidai kuwa mara nyingi alikuwa na CD ya albamu hiyo na alikuwa akiisikiliza mara kwa mara akiwa na washikaji zake.
Kabla ya kuanza rasmi ngumi za kulipwa, Joshua alikuwa amepigana mapambano 43 ya ridhaa, ambapo alipigwa mara tatu pekee. Lakini pia, kabla ya mwasumbwi alikuwa akifanya kazi za kubeba matofali katika shughuli za ujenzi.
Ondoka na Mkwanja Kwenye Tsh. 160,000,000
Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu.


Sabrina
Nyumbani ni nyumbani anajivunia kuwa muafrika
Povel
AFRICAN STAND up together 💪💪💪💪💪
Flomena
Good news
Amiri Kayera
Bondia mkubwa Sana Kwa sasa duniani
aisha
Huyu jamaa sasa ni.bondia wa dunia
Issa
Joshua ni bondia alieweka rekod nzur
Dorophina
Africa inavipaji vingi sana pongezi kwake
magdalena
kijana ana nyota kali sana uyu
Angelina
Goodnews
Zeiyana
Madawa ya kulevya yamewasili sana vijana ndoto zao wengi zimepotea
Caroline
Kumbe ni mnigeria.sikuwahi kujuaa
Lydia Emmanuel Magoti
Huyo ni bondia mwenye lekodi zake kafanya mahajabu mengi mno kwenye mapambano yake
Tatu
Joshua ni bondia nzuri ila slialikiwa na madawa ya kulevya
warda
Dogo huwa namkubali sana
Shani
Joshua ngum jiwe
Elika
Dogo anajiamini sana
Khadija
Anajiamini sana huyo dogo
Fatuma kasomo
Gud news
Hopemwaikuka
Joshua namkubal sana
Gabriel
Joshua ni bondia alieweka rekod
felister
bondia mkubwa sana kwa ss
Sauda
Anajivunia asili yake
Mwajumah
Namkubaligi sana uyu dogo
Ernest
Hard work always pays