Mashabiki wa mchezo wa masumbwi au ndondi kwa lugha ya kizungu wanaita Boxing, wanatamani kuona Anthony Joshua akipambana na Tyson Fury, promota wa Fury – Frank Warren anasema hii inawezekana.
Kwa muda mrefu kumekuwa na msukumo mkubwa kutoka kwa mashabiki wa mchezo wa ngumi wakitaka kuwaona wababe wawili wa Kiingereza wakipambana ndani ya ulingo mmoja.
Anthony Joshua ambaye anamkanda wa IBF, WBA na WBO anamtambia Tyson Fury ambaye ni bingwa wa dunia akiwa na mkanda wa WBC. Mchezo wa Joshua vs Fury umeendelea kuchagizwa na ushindi wa Joshua vs Kubrat Pulev ambapo alishinda kwa K.O siku ya Jumamosi.

Warren anasema “kama itatokea, utakuwa ni mchezo wenye pesa ndefu takribani euro milioni 300-500 zinaweza kupatikana, itategemea unachezwa wapi na lini. Timu zote zitapaswa kuweka pembeni majivuno.”
Promota wa Joshua – Eddie Hearn ameongeza kuwa “itachukua siku kadhaa kukamilisha mazungumzo na mchakato mzima kati ya wapiganaji hao.”
Japokuwa, ili mchezo huu utokee – kuna mambo kadhaa ya kufanyia kazi. Kuna wachezaji ambao wanasubiri mapambano yao dhidi ya Joshua na Fury.
Kwa upande wa Fury, atapaswa kurudiana na Deontay Wilder kwa mara ya tatu wakati ambapo Joshua ataelekezwa na WBO kupambana na Oleksandr Usyk ambaye ni mpinzani wake kwenye mkanda huo.

Pia kuna suala la wapi mchezo huo utachezwa pamoja na suala zima la urushaji wa matangazo ya mchezo huo kwa upande wa vyombo vya habari.
Sanjari na haya, Frank Warren anasema “inahitaji utendaji kazi wa pamoja ili kufanikisha mechi hii ambayo mashabiki wanataka kuiona.
“Ninauhakika itatokea. Wachezaji wanataka itokee na sisi kama mapromota na mameneja ni kazi yetu kuhakikisha inatokea. Ningependa ifanyike Uingereza lakini kwa sasa hakuna uwezekano huo kutokana na taratibu za COVID19, labda mpaka Juni mwakani.”
Endapo Joshua na Fury watachukuana, huu utakuwa ni mchezo wa kihistoria ambapo mikanda yote itawekwa mezani na mshindi ataibeba yote!!!
BURUDIKA NA WANYAMAPORI WAKIIMBA NA KUPIGA VYOMBO VYA MUZIKI!
Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, furahia mchezo wa Forest Rock. Hapa utaburudika na umahiri wa wanyapori wanaoimba na kutumia vifaa vya muziki wa rock. Burudika huku ukijiwekea nafasi ya kutengeneza pesa ndefu kupitia Meridianbet!!



Lydia Emmanuel Magoti
Vizuri lazima lazima iwezekane
Dorophina
Wakikutana mtanange wake utakuwa sio wa kitoto
Rahma
Hasnte kwa makala
Ernest
Itakuwa bonge la pambano
Mwanahamisi
Lazima kieleweke
Shakila mrope
Mpambano mkali san
Janeflora malisa
Asnt kwa taarif meridianbet
Saupha mohamed
Pambano kali sanaa
Khadija
Lazima kieleweke kila mtu anataka kuonyesha umwamba kwa mwezake
Sarah
Mpambano itakuwa mkali sana
Hopemwaikuka
Can’t wait for this
Issa
Itakua bonge la pambano
samiah
Pambano lakibabe
Tatu
Ponge la pambano
warda
Mashabiki wanataka kuona ngumi zenye mvuto