Beki wa Barcelona Dani Alves amesema kwamba angeweza kutumia kiasi kikubwa cha pesa kumsajili mchezaji Kylian Mbappe na siyo Erling Haaland.
Alves alisema kwamba Mbappe ni mchezaji aliyekamilika na wachezaji wote wawili wamekuwa wakihusishwa na kujiunga na klabu ya Real Madrid kwa kiasi kikubwa.
Mbappe ambaye amekuwa kwenye vichwa vya habari kuhusu kutimkia Bernabeu mwisho wa msimu huu tayari amefunga mabao 28 na kusaidia mengine 17 katika michezo 38 kwenye mashindano yote msimu huu.
Wakati Haaland ambaye amekabiliwa na majareha mengi msimu huu amefunga mabao 23 na kutoa asisti sita msimu huu akiwa na Dortmund.
Alves anaamini kama Barcelona wakitaka kusajili moja kati ya wachezaji hao basi Mbappe atapata kipaumbele kikubwa.
Akiongea na Sport Alves alisema: ” Mbappe ni mchezaji aliyekamilika kuliko Haaland katika idara zote.”
“Ningetumia pesa nyingi kwa Mbappe na siyo kwa Haaland.