Azpilicueta Anasalia Darajani?

Kocha mkuu wa klabu ya Chelsea Thomas Tuchel anaamini nahodha wa timu Cesar Azpilicueta anaweza kuongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo ya London.

Azpilicueta Anasalia Darajani?

Wakati mabadiliko ya umiliki wa Chelsea yakiwa bado yamekwama, Azpilicueta ametimiza idadi ya michezo iliyopaswa kuongezwa moja kwa moja kwenye mkataba, lakini makubaliano yake ya mdomo juu ya kuweza kuamua mustakabali wake yalikuwa na utawala wa Roman Abramovich.

Mhispania huyo, huku kukiwa na hali ya sintofahamu, anasubiri kujua kama watatimiza ahadi yao lakini kocha mkuu Tuchel anaamini kuwa nahodha wake ndiye aliyeanzisha kipengele ambacho kitamfanya abaki kwa mwaka mwingine.

“Ni habari njema kwetu,” Tuchel alisema kuhusu Azplicueta kucheza idadi ya michezo iliyoainishwa kwa ajili ya kuongezewa mkataba wake katika mkutano na waandishi wa habari.

“Tuna mkataba, ni nahodha wetu, kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa sana kwamba atabaki.”


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

Acha ujumbe