Bellingham Apigwa Faini na FA ya Ujerumani

Jude Bellingham amepigwa faini ya Euro 40,000 na Shirikisho la Soka la Ujerumani (DFB) kwa maoni yake kuhusu mwamuzi Felix Zwayer baada ya Borussia Dortmund kufungwa katika Bundesliga dhidi ya Bayern Munich.

Bellingham Apigwa Faini na FA ya Ujerumani

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza ameshtakiwa kwa “tabia zisizo za kimichezo” na amekubali adhabu yake.

Bellingham, 18, alitilia shaka uteuzi wa Zwayer, ambaye alifungiwa kwa miezi sita mwaka 2005 kwa kashfa ya upangaji matokeo, baada ya baadhi ya maamuzi yenye utata katika kupoteza kwa timu yake 3-2.

Zwayer alikataa rufaa ya Dortmund ya kutaka penalti na baadaye akawapa Bayern mkwaju wa penalti baada ya Mats Hummels kudhaniwa kuwa aliunawa mpira eneo la hatari.

Taarifa ya DFB ilisema: “Mahakama ya michezo ya Shirikisho la Soka la Ujerumani (DFB) ilimtoza faini ya euro 40,000 Jude Bellingham katika kesi ya hakimu mmoja baada ya kamati ya udhibiti ya DFB kuleta mashtaka kwa tabia isiyo ya kimichezo.

“Mchezaji wa klabu ya Bundesliga Borussia Dortmund tayari amekubali hukumu hiyo, hukumu sasa ni ya mwisho.

“Baada ya mechi ya Bundesliga dhidi ya Bayern Munich siku ya Jumamosi, Bellingham alisema katika mahojiano ya TV kuhusu mwamuzi Felix Zwayer: ‘Unampa mwamuzi ambaye tayari ana upangaji matokeo mchezo mkubwa zaidi nchini Ujerumani. Unatarajia nini?’.


AGENT JANE BLONDE AMEREJEA MSIMU WA SIKUKUU.

Unaweza kujishindia mamilioni katika kasino yako pendwa ya meridianbettz, mchezo wa Agent Jane Blonde Return ni moja ya michezo inayopendwa kwasasa huku ikiwafanya wachezaji kuwa mamilionea kila siku. Unasubiri nini! ungana na Agent Jane Blonde akufanye milionea.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

 

Acha ujumbe