Dortimund Haitafuti Mbadala wa Haaland.

Borussia Dortimund imeona hakuna uhitaji wa kufanya usajili kwaajili ya kupata mbadala wa Erling Haaland ambaye amekuwa na kiwango bora kabisa tangu atue klabuni hapo.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa kutoka Norway amekuwa wa moto tangu atue ligi ya Bundesliga mwezi Januari, amendelea kufurahia maisha akiwa Dortimund kama alivyokuwa Salzburg ikiwa tayari amefunga goli 16 katika michezo 18 hapo BVB.

Paco Alcacer ataachana na Dortimund atarudi tena kunako ligi ya LaLiga kujiunga Villarreal baada dirisha la usajili kufunguliwa.

“Hatujafunga magoli machache msimu huu,” Zorc aliiambia Kicker na vijana hao wa Favre wamefunga magoli 84 katika mechi 34 na wamemaliza msimu wa 2019-20 wa Bundesliga wakiwa nyuma kwa tofauti ya alama 13 nyuma ya wababe wa Bundesliga Bayern Munich.

Zorc anahisi safu ya ushambuliaji ya Favre ambayo inawachezaji machachari kama Jadon Sancho, Thorgan Hazard na kinda Giovanni Reyna ambayo imecheza katika kiwango kizuri kwa msimu wa 2019-20 inajitosheleza haina haja ya kuongeza mchezaji mwingine wa aina hiyo.

Haaland ameripotiwa kuongeza kifungu kwenye mkataba wake wa €75m na kusisitiza hatoondoka BVB ingawa timu za ulaya zimekuwa zikimtolea macho na mchezaji mwenzake Sancho amekuwa akionekana kutaka kuondoka klabuni hapo.

Winga huyo wa England amekuwa akihusishwa na kurudi katika ligi ya Premier League na Manchester United wameripotiwa kuvutiwa na mchezaji huyo.

Dortimund tayari wamejihakikishia huduma ya Thomas Meunier na kinda wa Uingereza Jude Bellingham.

 


 

Kwa sababu ya thamani ya pesa yako, kwa kila muamala unaofanya wa kuweka pesa kwenye akaunti yako ya Meridianbet unapata 5% bonasi.

Soma hapa zaidi

47 Komentara

    Kama wachezaji waliopo wanatosheleza timu hakuna aja ya Dortmund kusajili tena

    Jibu

    Haaland ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa sana.

    Jibu

    Asante kwa habari hizi za kujitosheleza

    Jibu

    Winga huyo wa England amekuwa akihusishwa na kurudi katika ligi ya Premier League na Manchester United wameripotiwa kuvutiwa na mchezaji huyo.

    Jibu

    Bora wasajili waongeze nguvu

    Jibu

    Ni sawa km kikosi kina mtu wa kukava nafasi ya jamaa haina shida

    Jibu

    si lazima kusajir ikiwa kama wanaona wako vzr

    Jibu

    Bora wasajili tu

    Jibu

    Kweli maana itakuwa matumizi mabaya ya Pesa

    Jibu

    dortmund hawawezag kabisa kukaa na wachezaji wazuri, ataishia bayern hyo siku si nying

    Jibu

    Kila nikisikia mchezaji Haaland namukumbuka wakala wake mwenye uchu wa fedha Mino Raiola ambaye wakati fulani Alex Ferguson aliwahi kumwelezea kama wakala hatari zaidi barani Ulaya. Mara nyingi Dortmund imekuwa ikipoteza wachezaji wake wazuri kuchukuliwa na Klabu kubwa zaidi#meridianbettz

    Jibu

    Watafanya vizuri wakisajili ili timu iwe nzuri

    Jibu

    Halaand yupo kwny msimu Bora Sana hv now

    Jibu

    Halland atafany makubw zaid

    Jibu

    Sioni kama kuna ulazima wa kusajili tena#meridianbett

    Jibu

    Halland Yuko vizur.Anawatosha.

    Jibu

    Ni vzr maan wanatumia bajet

    Jibu

    Kiukwel watakuwa wamefanya maamuz mazur maana ukiangalia bado wako vzur sana kwani Borussia Dortmund, au BVB, ni klabu ya kandada ya Ujerumani. Katika miaka ya karibuni, klabu hii imekuwa ni mpinzani mkubwa wa klabu ya Bayern Munich katika kinyanganyiro cha taji la Bundesliga.
    Borussia Dortmund wameshawahi kushinda Kombe la Shirikisho la Ulaya mwaka 1997 ambalo sasa linajulikana kama Champion’s Laeague pamoja na Kombe la washindi wa Ligi za Ulaya mwaka 1966 ambalo sasa linajulikana kama Europa League. Kiwanja chao cha mpira cha Westfahlenstadion ndio kikubwa zaidi katika ligi ya Bundesliga

    Jibu

    Dortmund wanawachezaji wazuri hakuna haja ya kuongeza wengine

    Jibu

    Wanawachezaji wazuri Dortimund

    Jibu

    Dortimundi anawechezaji wazuri na wanajitosheleza

    Jibu

    Maamuzi sahihi

    Jibu

    Erling halland ni mchezaj chipukiz hatar sana

    Jibu

    Maoni:wako sahihi kabisa

    Jibu

    Sijaona km wameongopa kwa hapo

    Jibu

    Hii ipo poa sana

    Jibu

    Wana majembe yakutosha

    Jibu

    Wasajili tu

    Jibu

    Ni wakati mgumu sana wanao Dortmund kocha kama kocha hawezi kuonyesha mazaifu yake mbele ya wachezaji kuondoka kwa haaland hameacha pengo kubwa Dortmund

    Jibu

    Haaland yuko vizuri itakuwa vizuri kama watapata sain yake

    Jibu

    Dortmund anawachezaji wazuri
    Naona Haina haja ya kuongeza

    Jibu

    Wanawachezaji wazuri sana Dortmund#Meridianbettz

    Jibu

    Bora wasajili waongeze nguvu

    Jibu

    Ni vizur pia

    Jibu

    Dortimund wana wachezaji wazuri mno#meridianbettz

    Jibu

    Kama wasipo sajiri mwingine kiwango si kitashuka

    Jibu

    Yuko sahihi

    Jibu

    Kama timu imejitosheleza usajili hauna haja

    Jibu

    Kama anawachezaji wakutosha aina haja ya kusajili# meridianbettz

    Jibu

    Yuko sahihi

    Jibu

    Wanajiweza Haina sababu ya kusajili tena

    Jibu

    Bora wasajili wachezaji wengine

    Jibu

    Inabid watafute mbadala endapo akaumia
    Itakua shida pia kwa timu

    Jibu

    Fresh tu

    Jibu

    Halaand bado hazivutii timu nyingi Sana Ndio maana hawapo tayari kutafuta mbadala wake

    Jibu

    Kweli Haaland Anajua sana#Meridianbettz

    Jibu

Acha ujumbe