Pep Guardiola amedai kuwa raia wa Uingereza wanataka Liverpool ishinde Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Manchester City ndiyo maana wanaisaidia timu hiyo.

Guardiola: Liverpool Inapata Sapoti na Kila Mtu Uingereza

Kikosi cha kocha wa, Manchester City kilisonga mbele kwa pointi tatu dhidi ya Liverpool kileleni mwa EPL kwa ushindi mnono wa 5-0 dhidi ya Newcastle United siku ya Jumapili.

“Kila mtu katika nchi hii anaunga mkono Liverpool … vyombo vya habari na kila mtu,” Guardiola aliambia beIN Sports.

“Bila shaka, kwa sababu Liverpool wana historia ya ajabu katika mashindano ya Ulaya.

“Sio kwenye Ligi Kuu, kwa sababu wameshinda moja katika miaka 30, lakini sio shida hata kidogo.”

Kocha wa Manchester City aliongeza kuwa hilo halimsumbui hata kidogo.

“Lakini sijali,” alisema.

“Wana wafuasi wengi duniani kote na Uingereza wanaunga mkono Liverpool zaidi kuliko sisi.”

“Tunahitaji kutafuta pointi tisa au labda sita hivi sasa, inategemea kile kitakachotokea katika michezo miwili ijayo kwa tofauti ya mabao, lakini sasa Jumatano ndiyo fainali ya kweli kwetu ugenini Wolverhampton Wanderers,” alibainisha. .

“Tutajaribu kushinda huko.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa