Harry Kane yuko mbioni kujiunga na Manchester City kutoka Tottenham Hotspur, Hii ni kwa mujibu wa The Sun, na ni hatua ambayo itamfanya nahodha wa England kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa katika Premier League. Hapa kuna wachezaji 10 wa juu zaidi wanaopata kipato katika ligi kuu ya Uingereza.
10. Edinson Cavani
Mshambuliaji wa Manchester United analipwa kiasi cha Euro 292,000 kwa wiki.
9. Anthony Martial
Mchezaji wa Manchester United anayecheza nafasi ya ushambuliaji analipwa Euro 292,000 kwa wiki.
8. Timo Werner
Mshambulaji wa Chelsea aliyesajiliwa kutoka RB Leipzig analipwa Euro 315,000 kwa wiki.
7. Paul Pogba
Kiungo wa Manchester United ambaye inasemekana hana mpango wa kuendelea na mashetani wekundu, analipwa Euro 338,000 kwa wiki.
6. Raheem Sterling
Winga wa Manchester City ambaye huenda akaondoka klabuni hapo wakati huu wa dirisha la usajili, analipwa Euro 350,000 kwa wiki.
5. Kai Havertz
Mchezaji wa Chelsea aliyesajiliwa kutoka Bayer Leverskusen analipwa Euro 362,000 kwa wiki.
4. Jadon Sancho
Winga wa Uingereza na usajili mpya wa Manchester United aliyekuwa akikipiga Borussia Dortmund atalipwa Euro 408,000 na Man United kwa wiki.
3. Pierre-Emerick Aubameyang
Mshambuliaji wa Arsenal na timu ya taifa ya Gabon analipwa Euro 408,000 kwa wiki.
2. Kevin De Bruyne
Kiungo wa Manchester City ndiye anayeongoza kwa kupokea mashahara mkubwa mpaka sasa Euro 449,000 kwa wiki.
1. Harry Kane
Mshahara ambao nahodha wa Uingereza anaripotiwa atalipwa kama akijiunga na Manchester City kutoka Tottenham Hotspur ni Euro 467,000 kwa wiki.
Kasino ya Mayan Eagle inakukufanya kuwa bingwa wakati wowote unapoamua kuicheza. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!



Ernest
Kweli City wamejilipua