Manchester United walikuwa wenyeji wa Aston Villa katika dimba la Old Trafford kwenye mchezo wa Premier League ikiwa imfika wiki ya sita na kuambulia kipigo cha 1-0 kutoka kwa vijana wa Dean Smith.

Huu unakuwa mchezo wa pili mfululizo kupoteza katika uwanja wa nyumbani baada ya kuchapwa 1-0 na West katikati ya wiki kwenye michauno ya Carabao Cup.
Katika mchezo wa leo Bruno Fernandez alikosa penati katika dakika za nyongeza penati waliyopata baada ya beki kuunawa mpira.
Mjadala uliyopo kwa wanasoka wengi sasa ni kwamba labda Christiano Ronaldo ndiye atakuwa mpiga penati baada ya Bruno kushindwa kuiokoa timu kwenye nafasi muhimu.
Goli la Hause lililofungwa katika dakika ya 88 lilitosha kwa upande wa Dean Simth kuondoka na alama tatu muhimu.
“Inawezakana wao walikuwa na nafasi nyingi kuliko sisi lakini tulikuwa na nafasi kubwa na tulikuwa tunastahili ushindi huu.” alisema kocha mkuu wa Aston Villa Dean Smith.
Ni wakati wa ushindi mkubwa ukiwa na kasino bomba ya Lock a Luck, meridianbet wanakupa sababu ya ushindi, funga bahati yako ya ushindi ukiwa na mabingwa.



Sania+mapua
Manchester united wanayumba