Staa wa Inter Lautaro Martinez amesema kwamba alikuwa karibu sana kuungana na Lionel Messi katika klabu ya Barcelona kabla ya kuamua kusalia San Siro.

Martinez: Nilikaribia Kuungana na Messi Barcelona

Martinez alikuwa akihusishwa na uhamisho wa pesa ndefu kwa kiasi kikubwa na miamba wa LaLiga kabla ya msimu 2020-21.

Baada ya dili hiyo ya kwenda Spain kuyeyuka Muargentina huyo aliamua kusalia Inter na hatimaye amefanikiwa kunyanyua taji la Scudetto wiki iliyopita.


“Kiukweli nilikuwa karibu sana kujiungana Lionel Messi Barcelona na niliongea hilo na Messi.” Martinez aliiambia ESPN Argentina.

Lakini The Blaugrana walikuwa na tatizo la kiuchumi kwa kipindi hicho, kwa hiyo nikaamua kubakia Inter. Na imethibitika yalikuwa maamuzi sahihi hasa baada ya kutwaa taji la Serie A.

Martinez alijiunga na Inter akitokea klabu ya Racingmwaka 2018 na mchezaji huyo wa miaka 23 amefunga mabao 47 kwenye mashindano yote akiwa na Inter yakijumuishwa 15 katika Serie A msimu huu.

Martinez alisema Real Madrid walijaribu kumsajili wakati akiwa katika klabu ya utotoni lakini mwishowe alijiunga na Inter.

“Real Madrid walikuja kunisajili lakini nilikataa na nilitaka nilikuze jina langu nikiwa Argentina kwanza kisha baadaye ndiyo niende Ulaya.


TENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO

Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!

SOMA ZAIDI


14 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa