Mashabiki wanahisi kwamba matokeo ya mechi ya jana kwa Manchester City yalichangiwa na Erling Haaland baada ya mshambuliaji huyo kutotumika kama mchezaji wa akiba katika sare ya 0-0 na Copenhagen kwenye Ligi ya Mabingwa siku ya Jumanne.
Haaland amefunga mabao 20 katika mechi 12 pekee msimu huu tangu ajiunge na City akitokea Borussia Dortmund msimu wa joto, lakini alipumzishwa na Pep Guardiola nchini Denmark, huku Manchester wakiwa tayari kufuzu kutoka kundi lao.
Manchester walipata bao la Rodri lililokataliwa baada ya mpira wa mkono uliopigwa na Riyad Mahrez katika maandalizi, wakati winga huyo wa Algeria akakosa penalti baadaye katika kipindi cha kwanza. Huku ikishindwa kupata mafanikio, mashabiki kadhaa walienda kwenye Twitter na kusema kwamba Manchester ilionekana kuhangaika bila Haaland.
‘No Haaland no party,’ shabiki mmoja aliandika kwenye mtandao wa kijamii.
Wakati huo huo, kulikuwa na ukosoaji mkali zaidi kutoka kwa shabiki mmoja ambaye alisema: ‘Manchester City haina maana bila HAALAND.’
Kuelekea mechi yao mjini Copenhagen, Manchester walikuwa wamefunga mabao 11 katika mechi zao tatu za awali za makundi, lakini hawakuweza kuzifumania nyavu wakati huu kwani walilazimika kugawana pointi moja.
Nae Shabiki mmoja alitania kwamba Manchester ilionekana kama gari la Williams F1 bila Haaland katika timu yao, akimaanisha timu ambayo kwa sasa iko chini ya msimamo wa mbio za magari ya Formula 1.
‘MAN CITY bila HAALAND ni kama gari la WILLIAMS F1,’ aliandika.
Manchester walipunguzwa hadi wachezaji 10 katika kipindi cha kwanza wakati Sergio Gomez alipopewa kadi nyekundu kwa kufanya madhambi alipokuwa mchezaji wa mwisho.
Guardiola kisha alipinga kishawishi cha kumleta Haaland baada ya mapumziko, licha ya kujua kwamba ushindi ungeihakikishia timu yake kutinga hatua ya 16 bora.