Mchezo wa Kirafiki wa Tanzania na Kenya Wafutwa.

Shirikisho la soka la nchini Kenya limethibitisha kufutwa kwa mchezo wa kirafiki wa Harambee Stars dhidi ya Taifa Stars.

Mchezo wa Kirafiki wa Tanzania na Kenya Wafutwa.

Mchezo huo ulipangwa kuchezwa katika dimba la Nyayo Stadium siku ya Alhamisi, lakini baada ya kuthibitishwa kwa kifo cha Rais wa jamuhuri wa muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli, shirikisho limethibitisha mchezo hautachezwa kama ilivyokuwa imepangwa.

Kiongozi huyo wa Tanzania kwa mujibu wa makamu wa rais Samia Suluhu,alikuw akisumbuliwa na tatizo la moyo katika hospitali ya jijini Dar es salaam kutoka March 14

“Kufuatia kifo cha ghafla cha Rais wa Tanzania, Mheshimiwa John Pombe Magufuli, Shirikisho la Soka Kenya, kwa kushauriana na Shirikisho la Soka la Tanzania, imefanya uamuzi wa kufuta mchezo wa leo wa kimataifa wa kirafiki kati ya timu ya kitaifa ya Harambee Stars na Taifa Stars, ambayo ilipangwa kufanyika katika Uwanja wa Kitaifa wa Nyayo, kuanzia saa 3:00 jioni, “taarifa ya FKF ilisomeka.

“Kwa niaba ya FKF na ushirika mzima wa mpira wa miguu Kenya, nawatakia amani na faraja katika nyakati hizi ngumu.”

Harambee Stars na Taifa Stars zilipangwa kucheza mechi ya pili ya kirafiki wakati zinajiandaa na mechi zijazo za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika. Mchezo wa kwanza, uliochezwa Jumatatu, ulimalizika kwa 2-1 kwa kupendelea upande wa Jacob ‘Ghost’ Mulee.

Kenya imepangwa kukabiliana na Misri na Togo katika mechi za kufuzu zilizobaki wakati Kim Poulsen anatakiwa kukutana na Equatorial Guinea na Libya.


Maana Kamili ya Ushindi Katika Kasino za Meridianbeti ni Pamoja na Mchezo wa Tropical Wild.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Tropical Wild na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

CHEZA HAPA

8 Komentara

    Ni kweli tuko kwenye majonzi

    Jibu

    Ni kweli kabisa ili ni pingo kubwa kwa Taifa

    Jibu

    Vizuri kwasababu Tuna msiba mzito Sana akunajinsi ishatokea

    Jibu

    Dahh inauma sana

    Jibu

    Tumepata pigo kubwa sana

    Jibu

    Tumepata pigo kubwa mno

    Jibu

    Tumepoteza shujaa mpambanaji wa wanyonge wamefanya vizuri kuhairisha mechi

    Jibu

    Tupo kwenye majonzi sana

    Jibu

Acha ujumbe