Christiano Ronaldo ataukosa mchezo EPL wa Manchester United dhidi ya Liverpool siku ya Jumanne baada ya kufariki kwa mtoto wake wa kiume baada ya kuzaliwa klabu yathibitisha.

Siku ya Jumatatu nyota huyo wa Ureno alitangaza taarifa za kufiwa kupitia akaunti yake ya Instagram lakini pia alibainisha kwamba mtoto wa kike amezaliwa salama na anaendelea vyema.

Ronaldo na mchumba wake Georgina Rodriguez walikuwa wakitarajia kupata mapacha, lakini waliomba faragha baada ya kupoteza na United sasa wamethibitisha kuwa Ronaldo atachukua muda wa likizo ya huruma.

Taarifa kwenye tovuti yao ilithibitisha habari hiyo, inayosema: “Familia ni muhimu zaidi kuliko kila kitu na Ronaldo anawaunga mkono wapendwa wake katika wakati huu mgumu sana.

“Kwa hivyo, tunaweza kuthibitisha kwamba hatashiriki katika mechi dhidi ya Liverpool kwenye uwanja wa Anfield Jumanne jioni na tunasisitiza ombi la familia la faragha.

“Cristiano, sote tunakufikiria na kuwapa nguvu kwa familia.”


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa