Mashindano ya Europa Laegue yanaendelea siku ya leo ikiwa ni hatua ya 16 na mechi zote nane zitachezwa siku ya Alhamisi na Manchester United watakuwa wakiwaongoza AC Milan katika dimba la Old Trafford.
Manchester United wanatarajia kucheza bila uwepo wa mshambuliaji wao Marcus Rashford na Edinson Cavani kwa mchezo huo wa mtoano ambapo mshindi atasonga kwa hatua ya robo fainali.
Rasford alitolewa katika mchezo wa wikendi dhidi ya mahasimu wao Manchester City baada ya kuumia kifundo cha mguu.
Wakati huohuo mshambuliaji mwenzeka Cavani ambaye alikosa mchezo wa debi atakosa mechi ya leo baada ya kusumbuliwa na maumivu ya misuli.
Mlinda mlango Dean Henderson atacheza tena kwa mara nyingine baada ya golikipa namba moja David de Gea kuwa nchni kwao Spain alikokwenda kuungana na mchumba wake ambaye amejifungua mtoto wake wa kwanza.
Straika Zlatani Ibrahimovic hatokabiliana na timu yake ya zamani baada ya kusumbuliwa na maumivu ya paja na mkongwe huyo ni mchezaji muhimu ambaye atakosekana.
Timu hiyo ya Italia itasafiri bila Theo Hernandez, Ismael Bennacer, Hakan Calhanoglu, Ante Rebic na MarioMandzukic.
Diogo Dalot ambaye yupo Milan kwa mkoo akitokea United yupo sawa kwaajili ya kuikabili klabu mama yake.
Kikosi kinachoweza kuanza kwa Man United (4-2-3-1): Henderson; Wan-Bissaka, Bailly, Maguire, Telles; Fred, Matic; Greenwood, Bruno Fernandes, James; Martial
Kikosi kinachoweza kuanza kwa Milan (4-2-3-1): Donnarumma; Calabria, Kjaer, Romagnoli, Dalot; Tonali, Kessie; Saelemaekers, Diaz, Castillejo; Leao
Ni Burudani Iliyokithiri na Mkwanja Nje Nje Katika Mchezo Halisi wa Chicago Gold.
Fanikisha malengo yako bila kuumiza kichwa, tengeneza mkwanja bila wasiwasi na kasino ya Meridianbet. Jiunge sasa Ufurahie Chicago Gold kasino.



Rahma
Uchambuz mzuri
Lydia Emmanuel Magoti
Huchambuzi uko vizuri
Hopemwaikuka
Umeeleweka
Caroline
Mambo ni moto
warda
Man united sijui kama watatoka ila mpira ni mambo ya bahat
Neema juma
Uchambuzi uko biyeee
Adelta
Mambo yanazidi kunoga
Sarah
Umesomeka
Angelina
Niceupdate
Issa
Wababe hawa