Mchezaji wa zamani wa Manchester United na Real Madrid Ruud van Nistelrooy amesaini dili ya mkataba wa miaka mitatu ya kuwa kocha mkuu wa klabu ya PSV Eindhoven kwa msimu ujao klabu imethibitisha.
Van Nistelrooy ambaye aliwahi kuitumikia timu ya taifa ya Uholanzi atachukua majukumu ya kuinoa PSV ambayo pia aliwahi kuichezea kwa miaka mitatu 1999 mpaka 2001. Van atachukua mikoba ya Roger Schmidt ambaye mktaba wake na klabu hiyo unaelekea mwisho msimu huu.
“Nimekuwa nikifanya kazi kwa wakati huu kwa miaka,” Van Nistelrooy alisema katika taarifa. “Ninajivunia na kushawishika kuwa niko tayari kuchukua nafasi ya uongozi katika klabu yangu. Mambo kadhaa yalikuja pamoja katika mwezi uliopita. Mazungumzo na wasimamizi wote na bodi yameimarisha maoni yangu juu ya umoja na nia ya kufikia kitu maalum na PSV kwa muda mrefu.
3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!
Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.