Jesse Lingard alicheza mchezo wake wa kwanza kwa timu ya West Ham tangu ajiunge na klabu hiyo mwezi uliyopita akitokea Manchester United kwa mkopo na alikuwa sehemu ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Aston Villa siku ya Jumatano akifunga mabao mawili.

Amekuwa wa pili kwa timu hiyo kufunga mara mbili kwa mchezo wa kwanza Premier League katika klabu hiyo ya West Ham baada ya Trevor Sinclair dhidi ya Everton mwezi Januari mwaka 1998.
Na kocha David Moyes hakuaacha hilo lipite hivi hivi kwani anaamini mchezaji huyo anaweza kumshawishi kocha wa timu ya taifa ya England kumuita katika kikosi cha timu ya taifa
“Nadhani bado ataendelea kutumika katikatimu yetu na tutamtumia, tumfurahishwa kwa sababu ameonesha tofauti,” kocha West Ham aliiambia BT Sport.
“Kama ataendelea na kasi hiyo aliyoionesha usiku wa leo haitachukua muda mrefu kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa.
Mchezaji huyo wa miaka 24 wa Uingereza mara ya mwisho kuichezea timu ya taifa ilikuwa ni katikati ya mwaka 2019 na Moyes anaamini kiwango alichoonesha dhidi ya Villa inaweza kupelekea kuitwa katika timu ya taifa kwa mara nyingine.
Neptune’s Richies ni mchezo Unaokupa pesa chap chap huku ukiwa unaburudika kupitia Kasino ya Mtandaoni ndani ya Meridianbet.



Adelta
West ham wako vizuri
Magdalena
West Ham wamejua kuucheza mpira
Rahma
Pongez kwenu West Ham
Caroline
Hongera Lingard..
Sania
Lingard ameanza vizuri
Dorophina
Lingard jembe jamaa anajua sana
Khadija
Wameanza vzr west ham
Venerose
Westham nawakubal
Mwanahamisi
Pongezi kwao
Ernest Kimeru
Jesse Lingard ameanza vizuri huenda ukawa mwanzo mzuri na muendelezo wa kuwa kwenye form
Lydia Emmanuel Magoti
Safii Sana pongezi kwao
David Pere
Lingad Amekuwa wa pili kwa timu hiyo kufunga mara mbili kwa mchezo wa kwanza Premier League katika klabu hiyo ya West Ham baada ya Trevor Sinclair dhidi ya Everton mwezi Januari mwaka 1998.
Issa
United mnakwama wap
Hopemwaikuka
Nmewakubal
Sarah
Pongezi kwake
warda
ilikuwa balaa