Pembeni yangu hapa nimetoka kukifunga kitabu cha Juddy Donnely. Kinaizungumzia safari ya binadamu watatu wa kwanza kwenda mwezini. Haikuwa safari nyepesi. Walitumia zaidi ya miaka 20 kuiandaa. Wakatumia miaka tisa kuishawishi serikali ya Marekani kuwapatia kibali. Baada ya mapigano mengi, hatimae waliruhusiwa na waling’oa nanga July 20 1969.
Haikutegemewa kuwa watarudi hai. Ila baada ya siku nne walitua salama pale Kaskazini mwa bahari ya Pacific. Mpaka leo majina yao wale binadamu yamesimama kwenye kuta za majengo ya NASA pale Washington DC. Neil Armstrong, Edwin Aldrin na Michael Collins. Nawaweka kando hapo kisha naufungua ukurasa wa Alphonso Davies.
Wazazi wake waliikimbia Liberia baada ya vita kupamba moto mwaka 1999. Hawakuwa tayari kushika bunduki kwa ajili ya kutetea maisha yao. Hawakutaka kuendelea kupishana na maiti barabarani. Hawakutaka kuendelea kusikia sauti ya mabomu. Wakaamua kuondoka na kuishia Ghana Magharibi katika kambi ya wakimbizi. Huko ndipo walipompata Alphonso mwezi November mwaka 2000.
Baadae walipata mfadhili wa kuwatoa katika kambi ya wakimbizi, wakaondoka kwenda Canada, Alphonso akiwa na miaka 5. Huko ndipo alipoanza maisha. Kwa kuwa wazazi wake hawakuwa na hela ya kumpeleka katika academy ya soka, alilazimika kuchezea timu ya kuwalea watoto wa mtaani kila jioni alipotoka shule. Soka lake likaanzia hapo.
Hapo ndipo alipoonekana na Vancouver Whitecaps, wakamchukua na kumpeleka katika academy yao. Baadae akapanda timu ya wakubwa. Bayern wakafanikiwa kumsajili July 2018 baada ya rais wa Barcelona kugoma kumsajili kwa kigezo kwamba hatokei taifa lenye historia ya soka. Ndiyo huyu Alphonso Davies tunayemuona leo kule kushoto kwa Bayern Munich.
Safari ngumu namna gani. Kutoka kupanga foleni ya chakula katika kambi ya wakimbizi hadi kuwa mchezaji bora chipukizi wa Bundesliga. Kutoka kucheza mitaani Canada hadi kupigwa buti na Lionel Messi. Safari ambayo kimawazo isingewezekana kufanikiwa kama ile ya kwenda mwezini.
Drops and Wins!
Umeijua hii? Ni promosheni kabambe ya ushindi kwenye Casino ya mtandaoni ya Meridianbet! Unaweza kushinda hadi Euro 2,000,000 leo.


Povel
Davis kijana mpambanaji Sana huyo anaonyesh ukomavu kwny soka na anahutendeah haki upande wake wa kushoto anastail tuzo ya mchezaj chipukiz wa UEFA Kama tuzo zitakuwepo msimu huu
Theckla
Anajua xana
Shafii
Alphonso Davis kwa kiwango ambacho amekionesha kwa sasa inaonesha kua amepitia magumu mengi na sasa alipopata nafasi niwakati wake wa kuomesha kiwango chake .
Mwajumah
Davis anajua sana kwa kiwango ambacho amekionyesha#Meridianbettz
Sauda
Anastahili tuzo..
Zeiyana
Histor yake ya maisha aliyo pitia ndio inamfanya hapambane sana ili kufikia ndoto zake.big up sana Davis tuna tegemea mengi makubwa kutoka kwako
Dorophina
Davis yupo vizuri sana na kiwango chake cha kuchezea ligi kubwa
Zeiyana
Histor yake ya maisha aliyo pitia ndio inamfanya hapambane sana ili kufikia ndoto zake.big up sana Davis
Ernest
Mtu adi kufikia mafanikio fulani lazima atakuwa amepitia mambo mengi sana, Ni wakati wake sasa kushine
Fatina mfingi
Davis anajua San kwa historia yake hiyo na ukitaka kufikia ndot zako inapidi ukubali changamoto
Ester jackson
Anastahili tunzo mana mafanikio yake yanaonyesha kuwa hakuna mafanikio yanayokuja kwa urahisi ni kuoambana hata kama ikiwa katika hali ya chini bado unaweza kuwa juu good job
Khadija
Anastahili tunzo maanamafanikio yake yanaonyesha kuwa hakuna matanikio yanakuja kwa urahisi lazima upambane sana ndio uje kufanikiwa
aisha
Davies yuko vizuri anajua sana
Adelta
Anastahili kupewa tuzo
@meridianbettz
Mwanahamisi
Anastahili tuzo
Magdalena
davies ana historia nzuri sana katika mpira
Lydia Emmanuel Magoti
Yupo vizuri Anastairi kwanacho kifanya
Saupha mohamed
Anastahili tunzo
Salma ngende
Yupo vizuri
Furahav
Kweli maisha km mlima kupanda na kushuka.
Gabriel
Alphonso Davies historia yake iko vzur sana
Johnmary joel
Anastahili#meridianbett
Amiri Kayera
Mda wake sasa
Sabrina
Alphonso yupo vizur
Devotha
Anastahili tuzo
Sadick
Ni historia ya kusisimua sana na Alphonso Davies alisema Baba yake alimufanya aipende Chelsea kwa maneno mengine moyo wake upo Stamford Bridge#meridianbettz
Janeflora malisa
Anastahil
Theonestina
Yuko vizur
David Pere
Hapo ndipo alipoonekana na Vancouver Whitecaps, wakamchukua na kumpeleka katika academy yao. Baadae akapanda timu ya wakubwa. Bayern wakafanikiwa kumsajili July 2018 baada ya rais wa Barcelona kugoma kumsajili kwa kigezo kwamba hatokei taifa lenye historia ya soka. Ndiyo huyu Alphonso Davies tunayemuona leo
warda
Maisha haya yanahitaji uvumilivu sana
felister
Huu ndiyo wakati wake sasa
Hope mwaikuka
Anaweza sana