Klabu ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck leo Agosti 22, imeibuka na ushindi wa mabao 6-0 mbele ya Vital’O ya Burundi kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Mchezo wa leo ulikuwa na lengo la kutambulisha wachezaji wapya pamoja na jezi itakayotumika kwa msimu wa 2020/21.
Ushindani ulikuwa mkubwa kipindi cha kwanza ambapo iliwabidi Simba wasubiri mpaka dakika ya 43 kupata bao la kwanza kupitia kwa Bernard Morrison ambaye alimaliza kazi ya pasi ndefu ya Larry Bwalya ambaye naye ni nyota mpya wa Simba.

Dakika mbili mbele, Morrison alitengeneza pasi kwa nahodha wa Simba John Bocco ambaye alipachika bao la pili dakika ya 45.

Simba ilikwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-0 huku Vital’O ikiwa haijaambulia bao ndani ya dakika 45.
Kipindi cha pili, Simba ilifanya mabadiliko kwa wachezaji wake wote ambao walianza kikosi cha kwanza ambao ni Aishi Manula, Shomari Kapombe, Gadiel Michael, Ibrahim Ame, Joash Onyango, Jonas Mkude, Hassan Dilunga, Larry Bwalya, John Bocco, Said Ndemla na Morrison.

Nyota walioingia ilikuwa ni pamoja na Beno Kakolanya ambaye aliumia dakika ya 64 na kumpisha Ally Salim, Mohamed Hussein,Keneddy Juma,Erasto Nyoni,Gerson Fraga,Mzamiru Yassin,Ibrahim Ajibu,Clatous Chama,Cris Mugalu, Charlse Ilanfya na Mirsaj Athuman.
Kikosi cha pili kilipachika mabao manne ambapo bao la tatu lilipachikwa na Chama dakika ya 56 akimalizia pasi ndefu ya Ajibu ambaye alifunga bao la nne dakika ya 75 kwa pasi ya Chama kisha bao la tano likapachikwa na Mugalu dakika ya 77 kwa pasi ya Miraj huku msumari wa mwisho ukipachikwa na Ilanfya kwa pasi ya Mohamed Hussein.

Sven amesema kuwa ulikuwa ni mchezo mgumu na mzuri huku wachezaji wake wakionyesha kile ambacho amewafundisha jambo ambalo linampa picha ya kikosi chake kuanza kufanya vizuri ndani ya ligi na mashindano mengine.
Drops and Wins!
Umeijua hii? Ni promosheni kabambe ya ushindi kwenye Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet! Unaweza kushinda hadi Euro 2,000,000 leo.


Nasra
Kile kipigi sio cha kubahatisha aisee
Mwajumah
Simba walijua kumchapa mtu bhana sio kwa bao zile wametufurahisha sana mashabiki wao sasa watani wetu wa jadi wajiandae mwezi wa 9 tutakavyowachakaza #Meridianbettz
Caroline
Mmeenda kuleta timu mbovu.ili tuwaone vidume.tumewashtukiaaaa.timu uko kwao imeshuka daraja
Sauda
Jana walijua kubahatisha..
felister
kilikua cha kawaida tu
aisha
Simbaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa sitaki kusema mengi wenyewe waneona kuwa sisi ni watu wabaya jamani simbaaaaaaaaaaaa nasikia raha hadi nahisi kulia simbaaaaaaaaaa ni baba lao maana mambo yalianzia kwenye show tulimaliza kila kitu baraka zote zimeachwa n mondiiiiii
Tatu
Simba Jana wametufoke si kwa mabao yale
Fatina mfigi
Simba sio ya mchezo mchezo Yani tulijua tyu yang mtaongea Ila nn subir muone tumeleta Tim mbov au nn!!
Ester jackson
Kikubwa. Duwa tunataka wakutane na wajadi wao tuone mambo yakoje kutokana na usajili wao
farida ahmadi
Simba baba lao ni nouma Sana hakuna kama Simba
rama
Maoni:simba wana kikosi kizuri sana msimu huuu atari
Sadick
Nadhani ilitakiwa wafunge mengi zaidi maana kila kipindi walicheza wachezaji tofauti hivy walikuwa na ari mpya na nguvu mpya#meridianbettz
Khadija
Simba jana imenifurahisha sana mashabiki wa simba oyeeee#meridianbettz
Zeiyana
Me sioni haja ya leo simba kushangilia ushindi ambao timu umeichagua wenyew kucheza nayo na mmeilipa mwenyew ni sawa mwanamke hanunue mwanaume alafu Nazi hafanye mwenyew na ukiangalia timu yenyew uko kwao imeshuka daraja..!yani mashabiki wote wa simba jana walikua hawana hata haja ya kushingilia yani kama wamepasha misuli tu wanaomba dua hiyo siku wakikutana na wanaume ila mashabiki viele ele ndio wanao piga kelele
Adelta
Mashabiki wa simba Jana tulifurahi sanaaaaaaaaaaa@meridianbettz
Dorophina
Wamebahatisha amna lolote wamewaachia tu kwasababu mechi ilikuwa ya kirafiki
lombo
THIS IS SIMBA
Furahav
Simba haina mpinzani.
Isaya massawe
Simba sijaona ajabu kumfunga vital’o
Antony Luseno
Simba walitisha Jana hu moto waendelee nao msimu ujao
Lydia Emmanuel Magoti
Kabisa kile kibigo kilikuwa si chakitoto kilikuwa chambwa mwitu kwakweli Mambo yalikuwa moto huwanja wamkapa akuna Kama zimba mashabiki fulu kufurahi yani
Ernest
Kama namuona vile Baraka Mpenja akitangaza mauaji haya ya kikatili kutoka kwa Simba
Mwanahamisi
Simba aina mpinzani
Samiah
Simba haina mpnzani
Fatuma kasomo
Naipenda cmba mpo vizuri
Issa
Simba imepata mchekea tu jana
JULIANA
Simbaaaaaaa wamejipanga
Sabrina
Mmmh Simba wamekutana na vilaza tuu
Amiri Kayera
Simba wako vzur
Hope mwaikuka
Simbaaaa juuuu
Povel
This is SIMBA next LEVEL
Samira
Simba ni next level…jana walijua kutapa raha mashabiki zao
Saupha mohamed
Simba babalaooo
Neema
Haya bhana wanasimbaa tuwape hongera zenu khaa.mmetisha
Shafii
Hongera yao.
Latifa juma mohamed
jambo ambalo linaleta picha ya kikosi kuanza kufanya vizuri ndani ya ligi na mashindano mengine, hongereni wanasimba.
warda
Goli kama hizi anahitajika kufugwa Yanga#Meridianbettz
magdalena
simba wana kikosi kizuri sana na wanajituma sana na kinajituma sana tena sana sisi wanakamati tunaelewa
Salma ngende
Hongera yao
Gabriel
Simba hapo ni Kama wamejitekenya wenyewe na kuanza kucheka wenyewe hauwezi kumkarbisha mgen then umpatie kila kitu had hela alafu umwambie akupige
jullie
timu makini na watu makini big up
Rose kapinga
Simba kama simba wababe!!!
David Pere
Kama namuona vile Baraka Mpenja akitangaza mauaji haya ya kikatili kutoka kwa Simba
Tahiya
Simba baba laooo