Ni kama kocha mkuu wa Simba Sven Vandernbroeck amekubali yaishe Simba, na hii inatokana na interview ya jana mara baada tu ya ushindi wa 2-1 vs Namungo.
Mtangazaji alimuuliza Sven ni kwa namna gani amejiandaa na michuano ya mabingwa Afrika baada ya kubeba ubingwa, Sven akajibu “timu inabidi iwe kamili na iandaliwe vizuri na hilo litafanywa na kocha mkuu, awe ni mimi au hata kama hatakua mimi”.

Jibu la Sven lilimfanya muandishi kumuulia kwanini anasema “huenda atakua yeye au sio yeye” na kocha huyo akajibu kwamba amesikia yanasoyemwa na yeye ni muajiriwa tu hivyo yuko tayari kwa habari yoyote hivi sasa.
Kocha huyo amesema kwa sasa anachukua likizo na wakati huo wa likizo atatuliza akili yake huku akisikilizia kama viongozi wake watamuambia arudi au asirudi.

Hii inakuja siku chache baada ya tetesi kuanza kuzagaa mitandaoni kwamba Simba hawana mpango tena na Sven pamoja na kuwapa makombe mawili msimu huu, kawapiga Yanga 4, kawapa ubingwa wa Tanzania, kawapa FA, vipi aondoke?
Tiketi yako ya kwanza kamwe haiwezi kupoteza ukiwa na Meridianbet. Unarudishiwa 100% ya Tiketi yako ya kwanza.


Johnmary joel
Nimekukubali sana kujiamin ndo mpango mzima#meridianbett
Omary lukumbi
Mtu anapo fanya vzr haina budi kubaki nae maana mimi sion alipo kosea hali ya mapungufu ni jambo la kawaida kwa kila mwanadamu ila amefanya kazi mzr sana msimu huu
Theonestina
Uongozi nao inabidi wamfikilie.amepambana vyakutosha
Tatu
Asante kwa taarifa
Salma ngende
Hata kama awajaamua kumrudisha yupo vizuri hatapata sehem nyengine nzuri zaidi
Magdalena
Kocha yupo vizuri Sana SEMA sisi mashabiki haturiziki
aisha
Simba wanataka kuyumba wakimpoteza huyo jamaa maana msimu huu amefanya vizuri sana
felister
safi nimempenda kocha yupo tayari kwa lolote litakalotokea
Adelta
Kujiamini Ni kila kitu
@ meridianbettz
Mwajumah
Kocha makini sana#Meridianbettz
Dorophina
Msimu huu Sven amejitahidi sana angebaki tu simba
Issa
Bongo hamna mpira na vilabu hivi viwili ndio chachu ya hilo
Shafii
Maamuzi ya kumtoa kazini yapo chini ya uwongozi wa simba wao ndo wanajua mapungufu yake aliyokua nayo licha ya kuchukua vikombe vyote hivyo.
Khadija
Amejiani nini?#meridianbettz
Lydia Emmanuel Magoti
Kocha yupo vizuri anajua Nini anakifanya kwenye kazi yake alafu kilabina damu anamapungufu yake kwaio Kuna kukosea na kunakupata kwaiyo msiwe mnamjaji Sana atayeye binadamu kwaio wenye krabu yao ndio wenye uwamuzi Kama watamtaka tena hau raha yupo vizuri anapamba anajitaidi Sana
Devotha
Uwongozi ndo unamjua vizuri kocha wao
Rehema
Asante kwa makala
Ester jackson
Pongezi kwake pia hakuna binadamu asiye kosea na nikawaida kwa makocha kutolewa katika nafasi walizo Nazi katika timu haijalishi ulifanya vizuri Mara ngapi ila kama ukifanya makosa ya Mara kwa Mara au ukafanya kosa zaidi lazima utaondolewa tu hakuna timu inayotaka kusifiwa ujinga.# meridianbettz
Ernest
Sven Vandernbroeck bado ananafasi ya kudhihirisha kiwango chake cha ufundi kwenye mashindano haya makubwa ambayo Simba wanaenda kupambana
Sadick
Moja ya matatizo ya soka letu ni kubadili makocha kila uchao, tunapenda matokeo mazuri lakini mafanikio endelevu huchukua muda tena taratibu kuyapata. Pengine kuna mengine nyuma ya pazia ambayo hatuyajui#meridianbettz
Sabrina
Asante kwa taarifa za michezo na burudani
Janeflora malisa
Habar njm
jullie
usitufokee
jullie
imekaa poa
Leonard
Vilabu vyetu havikai n makocha hata wakiwapa mafanikio
Hope mwaikuka
Imeeleweka hyo
David Pere
Hiyo Ndio kazi ya ukocha Yani uhakika zaidi wa kazi ni mdogo wakati mwingine
Genia Sikaluzwe
Imekaa poa sana
Theonestina
Duuuh
Amiri Kayera
Tusubir week hii tutajua km yupo au la
Fatuma kasomo
Kocha makini sana huyu
Zeiyana
Kocha licha ya kuchukua makombe yote hayo inawezekana ana mgogolo na uwongozi wa simba.
Neema juma
Taarifa iko poaw
Angelina
Goodupdate
Gabriel
Nice update 😌
Caroline
Ha ha ha yupo tayari kwa lolote
warda
Matola na Seven wametisha sana#Meridianbettz