Mchezaji wa kimataifa wa Brazil Richarlison ametibitisha kwamba amemwambia Lampard na uongozi wa Everton kwamba yupo tayari kuachana na klabu hiyo akisema kwamba meneja na klabu wanajua nin anakitaka.

Fowadi huyo alikuwa mtu muhimu katika kuhakikisha kwamba timu hiyo haishuki daraja msimu uliyoisha wa EPL.

Everton baada ya kunusurika kushuka kwenda kucheza Championship sasa wanataka kuimarisha timu yao na watakuwa bize wakati wa dirisha la usajili la majira ya joto kwa kusajili wachezaji bora.

Lakini wakati wanataka kukiboresha kikosi chao tayari watawapoteza wachezaji muhimu kama Richarlison na Dominic Calvert-Lewin ambapo Richarlison amekuwa akihusishwa na vilabu kama Real Madrid, PSG, Bayern, na Manchester United ambako anaweza kucheza kwenye michuano ya Ulaya kuliko Everton.

Richarlison aliiambia Globo: “Tayari nimeshaweka wazi kwa bodi na tayari nimeshazungumza na Lampard na watu wangu.

“Wanajua ninachotaka. Wacha tusubiri Juni.


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa