Benzema, Messi, Mbappe Tatu Bora Mchezaji bora wa Mwaka

Wachezaji Karim Benzema, Lionel Messi na Kylian Mbappe wameingia kwenye tatu bora ya kinyang’anyiro cha kumtafuta mchezaji bora wa mwaka 2022 kupitia shirikisho la soka duniani.

Baada ya kutangaza lorodha ya mwisho ya makocha watakaowania tuzo ya kocha bora wa mwaka shirikisho la soka duniani FIFA wametangaza tatu bora ya wachezaji watakaowania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa kiume kwa mwaka 2022. Orodha hiyo imeongozwa na Karim Benzema, Lionel Messi na Kylian Mbappe.BenzemaWachezaji hao wamefanikiwa kuingia kweny kinyang’anyiro hicho baada ya kufanya vizuri zaidi mwaka 2022 na kuzisaidia timu zao kutwaa mataji mbalimbali kwa mwaka huo, Karim Benzema alifanikiwa kuchukua tuzo ya Ballon Dor akiisaidia Real Madrid kutwaa taji la La liga na kombe la ligi ya mabingwa ulaya huku kila kombe waliloshinda akiibuka kama mfungaji bora.

Mchezaji Lionel Messi yeye alifanikiwa kutimiza ndoto yake ya muda mrefu baada ya kufanikiwa kuiwezesha timu ya taifa ya Argentina kubeba kombe la dunia nchini Qatar, Huku akifanikiwa kunyakua tuzo ya mchezaji bora wa michuano hiyo lakini pia klabu yake ya PSG aliiwezesha kutwaa taji la ligi kuu nchini humo.BenzemaMshambuliaji Kylian Mbappe kwa upande wake alifanikiwa kua na mwaka mzuri sana akiisaidia klabu yake ya PSG kunyakua taji la ligi kuu nchini humo vilevile akimaliza kama mfungaji bora wa ligi hiyo, Lakini Mbappe pia aliisaidia timu yake ya taifa ya Ufaransa kufika fainali ya kombe la dunia na kuibuka mfungaji bora wa michuano hiyo.

Mchuano ni mkali sana katika orodha hiyo kwani kila mchezaji anaweza kutwaa tuzo hiyo kutokana na mafanikio ambayo ameyapata binafsi kwa mwaka 2022, Lakini pia kwa namna ambavyo wachezaji hao wameweza kuzisaidia timu zao kuweza kutwaaa mataji.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.