Fenkie De Jong amesema kwamba aibu ya kufungwa 8-2 na timu ya Bayern Munich kwenye mashindano ya Champions League siku ya Ijumaa imeonesha ni kwa kiasi gani kuna matatizo mengi ndani ya klabu hiyo ya Barcelona.
Barca waliruhusu kufungwa goli nane kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1946 katika michuano hiyo ya hadhi ya juu ulimwenguni na wababe wa Bundesliga Bayern Munich
Tunaweza kusema Bayern walimaliza mchezo ndani ya kipindi cha kwanza kwa kuweza kufunga magoli manne kwa moja kitu kilichofanya Barca wapoteane na kuruhusu magoli mengine manne katika kipindi cha pili cha mchezo na kufanya Barca watolewe katika hatua ya robo fainali katika Champions League kwa mara ya nne ndani ya misimu mitano.

Baada ya matokeo hayo inaripotiwa kuwa kocha Setien huenda akafukuzwa baada ya kufanya vibaya katika msimu na nyota wa Barcelona De jong ameeleza.
“Nadhani leo imejionesha kwamba tuna matatizo mengi ndani timu,” De jong ambaye huu ndiyo msimu wake wa kwanza ndani ya Camp Nou akisajiliwa kutokea Ajax, alisema “Nadhani usiku wa leo umeonesha na tunajua tunahitaji kufanya mabadiliko makubwa.
“Ni ngumu sana mashabiki wetu kutuelewa tunatakiwa tufanye mabadiliko ya vitu vingi sana.
“Tuliamini tutawapiga Bayern ndani ya dakika 15-20 kwa sababu walifunga goli mapema nasi tuka sawazisha na kupata nafasi mbili nzuri nafikiri uliona mwanzoni mwa mchezo.
“Lakini walikuwa wazuri kuliko sisi, sidhani kama ni suala la vipaji sana nafikiri ni kuweka nidhamu na kujituma tuna hitaji kubadilika.
Aliulizwa pia kama kuna timu yoyote ya kumzuia Bayern kati ya Manchester City au Lyon kwenye nusu fainali – Muholanzi huyo De jong alijibu: ” Nadhani City wana timu nzuri Lyon pia ni wzuri.
Umekuwa mteja muaminifu wa meridianbet? Kuna zawadi kibao hadi 5% ya pesa yako inarejeshwa kwako. Kila wiki unaweza kurudishiwa mpaka Tsh 250,000.


warda
Hakuna Matatizo Ni Basi tu Uwezo Unaanza Kushuka#Meridianbettz
Caroline
Pole yao
Njiku
Tatizo lipo kwa messi
Nasra
Siku hazifanani tu ila tatzo
Mwajumah
Uwezo ushaanza kushuka polen sana barcelona#Meridianbettz
Theckla
Barcelona wamekuwa na msimu mbaya sana
Mwanahamisi
Pole yao
Latifa juma mohamed
Ni ngumu sana kwa mashabiki kuelewa barcelonainabid wafanye mabadiliko ya vitu vingi sana.
Adelta
Barcelona wanahitaji nidhamu ya kujituma
Ili wawe imara@meridianbettz
Dorophina
Barca wameanza kushuka kiwango kwa sasa
Mariam mtandama
Duuuh
Ester mmakasa
Barcelona inasikitisha sana kwa hatua waliyofikia.
aisha
Duuh poleni sana barcelona ila sasa inabidi mjue mnakosea wapi
Sylvester
De Jong amesajiliwa kipindi si sahihi na Barcelona,ila bado ana umri mdogo akaze msuli asife moyo kwani bado wana muda wa kutengeneza kikosi upya
Ernest
Jana Barcelona were totally downgraded by Bayern
Sauda
Barcelona wameshuka kiwango
Tatu
Barcelona wanatakiwa wakae chini na kocha wao waangalie walipokosea wapi na pia wasitegemee MTU mmoja ndio aje kuinyanyua timu
Sadick
Kabla ya mchezo Bayern ilikuwa inatabiliwa kushinda dhidi ya Barcelona ilikuwa lakini si kwa goli nyingi kiasi hicho, kunahitajika mabadiliko makubwa pamoja na kuondoa wazee kama akina Gerrard Pique#meridianbettz
felister
hakuna cha matatizo wala nn ni mpira tu kubalini matokeo Barcelona wenzang 🤸🤸🤸
Lydia Emmanuel Magoti
Sikumoja moja sio mbaya mpira ukipo tea kwaio mjipange kipasavyo napenye makosa palekebishwe
Zeiyana
Tatizo Barcelona hawana kikosi kizuri wana staa tu messi na sio wachezaji na ukiangalia sana toka mapunziko ya korona wachezaji chupukizi ndio wamekuja na moto was hajabu..!messi hana uwezo sasa hivi mri nao ushaenda wangepanga usajili mkubwa kwanza ili kuimarisha timu yao daaaah…!
Shafii
Barca ametia aibu ulimwengu mzima ni magoli mengi Sana ukiangalia ni mashindano ya hadhi duniani de jong yuko sahihi barca wanahitaji mabadiliko makubwa Sana.
Samira
Yaani mi sijaamini timu kubwa kama Barcelona wanaweza kufungwa goli nyingi vile na kama kweli wameyaona hayo matatizo ndani ya timu wafanye kuyatatua mapema sana timu itakufa
Neema
Hiyo ni kama ajali barabarani. Tusiwalaumu sana
Fatina mfingi
Duuh
Janeflora malisa
Barcelona imekuwa aibu sana
Rehema
Kumbe bwana mkubwa alikuwepo anatia masela aiseee aibu Sana Messi duuuh
Khadija
jamani kazi ipo kwa barcelona
Povel
Barcelona wamekuwaha mwendelezo mbaya sana
Issa
Barca walipotea mechi hii bayern walitumia udhaifu wao na kumiliki sehemu ya kiungo sana
Saupha mohamed
Barcelona saiv hawana mabeki
Furahav
Barca hawana jipya tena.
Hope mwaikuka
Matatizo ndo sehem ya maisha
Revina
Matatizo ndo wanaona sasa ,baada ya kufungwa ,Timu ilisifiwa sana
Gabriel
Barcelona mabek hakuna kabisa
Devotha
Yani hii barcelona imekua utopolo fc
Salma ngende
Dah!!inaumiza sana
Omary lukumbi
Barcelona mbovu tuu msimu huu wachezaj wengi umri umeshaenda inabid kocha atakae kuja asiangalie majina fumua kikosi kizima ijenge timu upya sasa hv Barcelona ikifanya vibaya macho yote kwa.lionel messi
Venerose
Mmh
rama
Maoni:kwel kabisa
Ester jackson
Yuko sahihi ila kwa upande wangu sidhani kama kunatimu ya kumzidi Bayern jinsi uwezo wake ulivyo wamejipanga kiukweli ila tusubiri kuona nani atakuwa mbabe zaidi yake dk 90
Rose kapinga
Barcelona mnafeli wapi?
Samiah
MMmh
farida ahmadi
Sio yakulaumu hinatakiwa matatizo ya Barcelona kusuruhishwa
David Pere
Baada ya matokeo hayo inaripotiwa kuwa kocha Setien huenda akafukuzwa baada ya kufanya vibaya katika msimu na nyota wa Barcelona De jong ameeleza.
magdalena
barcelona kunaweza kukawa na tatizo tena kubwa maana kungekuwa hakuna tatizo wasingekubali kupata aibu kubwa kiasi kile
Theonestina
Pole yao