KOCHA Msaidizi wa Namungo, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amefunguka kuwa katika dirisha hili kubwa la usajili wamechukua wachezaji wazuri kwa ajili ya kuimarisha kikosi chao.

Akizungumzia maandalizi yao, Julio amesema kuwa tayari kikosi chao kimeanza maandalizi ya msimu ujao na kwa sasa wapo Jijini Dar.

“Tayari tumeanza mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya na hatuwezi kutamba kama wengine wanavyosema ila ligi itakapoanza ndio tutajua aliyejiandaa vizuri.

“Tumefanya usajili mzuri na tumeachana na baadhi ya wachezaji, maingizo mapya wapo saba ambao ni wa kigeni na nane wazawa.”


BASHIRI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa