OFISA habari wa Yanga, Hassan Bumbuli ameweka wazi kuwa wanajivunia ubora wa mastaa wapya waliosajiliwa ndani ya kikosi hicho kuelekea msimu ujao wa 2022/23 na kuweka wazi kuwa, hawana haja ya kujisifu sana bali wapinzani wao wajiandae kwa maumivu msimu utakapoanza.

Kuelekea msimu ujao uongozi wa Yanga umefanikiwa kukamilisha usajili na kuwatangaza mastaa wapya watano wa kimataifa ambao ni, Gael Bigirimana, Stephanie Aziz Ki, Joyce Lomalisa, Lazarus Kambole na Bernard Morrison.

Mastaa hao pamoja na wenzao tayari wamejiunga na kambi kwa ajili ya kuanza mazoezi ya kabla ya msimu ‘Pre-season’ yaliyoanza Jumamosi iliyopita kwenye viwanja vya mazoezi vya timu hiyo huko Avic Town, Dar.

Bumbuli alisema: “Tumeanza kambi ya kujiandaa na msimu ambapo kocha mkuu, Nasreddine Nabi anaendelea na progranu za mazoezi ambapo pia tunatarajiwa kuwa na michezo ya kirafiki kama sehemu ya maandalizi kabla ya ya Wananchi na kucheza mchezo wa Ngao ya Jamii.

“Kimsingi sisi hatuna kelele nyingi kwa kuwa tuna kikosi bora ambacho kimefanya vizuri msimu uliopita, lakini pia tumefanya usajili bora, hivyo wengine waacheni wapige kelele ila wajiandae kwa maumivu.”


BASHIRI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa