MATARAJIO ya wengi yalikuwa ni Yanga kuachana na straika wao, Yusuph Athuman kwenye dirisha kubwa la usajili jambo ambalo halijafanyika.
Yusuph Athuman ambaye alijiunga na Yanga akitokea Biashara United kwa msimu uliopita hakuonyesha kiwango kikubwa kama ilivyokuwa kwenye kikosi cha Biashara.

Yanga tayari imetangaza kuachana na wachezaji wake wanne huku jina la Yusuph likiwa halijatajwa.

Yusuph Athuman
Yusuph

Chanzo chetu kutoka Yanga, kimefunguka kwamba “Watu wengi walitarajia kuachwa kwa Yusuph Athuman kutokana na kiwango chake lakini imekuwa tofauti.

“Sababu kubwa ni kutokana na mwenendo mzuri mazoezini hata kwenye michezo ya kirafiki ile ya ndani iliyochezwa amefunga mabao saba akicheza nyuma ya Mayele (Fiston).

Mayele ndiye kinara kwenye michezo ya kirafiki akifunga mabao nane pia suala la umri ndilo lililombakiza Yanga hivyo endapo akipata nafasi ataonyesha kiwango kizuri.”


Kwa Habari na Uchambuzi Unaweza Kugusa Video Hii

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa