Lampard Amtaka Mertens

Frank Lampard amezungumza na mshambuliaji wa Napoli Dries Mertens kuhusu kijiunga na Chelsea. Lampard walikuwa na mpango wa kuboresha sehemu yake ya ushambuliaji katika dirisha la Januari lakini Chelsea hawakufanikiwa kusajili straika mpya.

Mertens, amefunga magoli 12 katika mechi 29 alizecheza msimu huu Napoli, amekuwa kwenue mawindo ya Chelsea. Lampard bado hajakata tamaa kumsaini straika huyo wa Ubeligiji.

Ripoti zinasema kuwa kuna mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Lampard na Mertens. Mkataba wa Mertens na Napoli unamalizika kipindi cha kiangazi lakini bado hajafanya mazungumzo yoyote na Napoli.

Kama Napoli hawatampa mkataba Mertens inawezekana akaondoka bure kwenda Stamford Bridge, baada ya mkataba wakw wa sasa kumalizaka.

2 Komentara

    Mchukueni jeshi huyo.

    Jibu

    Yuko vizuri mchukueni

    Jibu

Acha ujumbe