Lionel Messi, Christiano Ronaldo, Jose Mourinho, Pep Guardiola na Jurgen Klopp wote wanatakiwa katika LaLiga amesema rais wa ligi hiyo Javier Tebas.

 

Messi, Ronaldo, Guardiola na Klopp Wanahitajika LaLiga.
Lionel Messi na Christiano Ronaldo.

Hatima ya Messi imeendelea kuabaki ni maada muhimu ya kushughulikiwa na miamba ya LaLiga baada ya kuomba kuondoka klabuni hapo kufuatia kashikashi za msimu 2019-20.

Mshindi huyo wa tuzo ya Ballon d’Or mara sita alikuwa akihusishwa na kujiunga na klabu ya Manchester City inayoshiriki ligi ya Premier League kabla hajaamua kusalia Spain, ingawa pia amekuwa kihusishwa kujiunga na kalbu ya Ligue 1, Paris Saint-Germain.

Tebas aliulizwa kuhusu hatima ya Messi na aliulizwa kama kunauwekano wa Muargentina huyo kuondoka upo.

“Namtaka Messi katika LaLiga, kama ninavyomtaka kocha wa Tottenham Mourinho, Pep Guardiola, bosi ya Liverpool Klopp na supa staa wa Juventus Christiano Ronaldo…,”Tebas alisema katika kilele cha mkutano wa World Football Summit. “Wote wanakusaidia kukua.

Messi, Ronaldo, Guardiola na Klopp Wanahitajika LaLiga.
Pichani Pep Guardiola, Jurgen klopp na Jose Mourinho.

“Sioni kama ina mantiki, watu wanapo sema kuwa hawana umuhimu. Neymar aliondoka, ni muhimu kuwa na mikakati mchezaji anaweza kukusaidia.

“Ni matumaini yangu kuwa Messi ambaye ni mchezaji bora wa dunia wa muda wote atamalizia soka lake hapa.

Messi ametumia maisha yake ya soka kuwa Camp Nou, ambako alijiunga na timu ya vijana ya Barcelona mwaka 2004.

Tangu aanze kuichezea Barca Messi amekuwa mfungaji bora wa Barcelona wa muda wote akiwa amefanikiwa kushinda mataji 34 ukijumuisha mataji kumi ya LaLiga na manne ya Champions League.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

17 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa