JUMA Mgunda Ramadhan, kocha wa muda wa Simba SC amesema kuwa suala la kuwa ataendelea kubaki kwenye timu hiyo au ataondoka litakuja kufahamika baadae kwa sasa anachoangalia ni kufuata maagizo ya viongozi.
Mgunda Afunguka Maisha Yake Mapya Ndani ya Simba
Kocha Mkuu wa Simba SC-Juma Ramadhan

Mgunda alisema anachojua ni kuwa kuna majukumu ya muda ambayo amepewa na viongozi wa klabu hiyo na sasa anajiandaa ili kupambana na Tanzania Prisons ugenini  kesho kutwa Jumatano kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya.

Juma alisema kuwa: “Kila kitu kitakuwa sawa baada ya muda kama nitaendelea kubaki kwenye timu au itakuwaje. Muda ni rafiki mzuri sana wa kila kitu.

“Ninachojua viongozi kuna vitu wanahitaji kutoka kwangu na nasikiliza wao wanataka nini kutoka kwangu. Tumetoka Malawi na sasa tunajiandaa kwenda Mbeya kwa ajili ya mechi yetu na Prisons.

“Baada ya hapo tutarudi kwa ajili ya mechi yetu ya marudiano na Nyasa Big Bullets, hivyo hayo ndiyo yaliyopo sasa. Hayo yakuwa nipo au sitokuwepo tusubiri wakati wake.”Alisema Juma

Mgunda Afunguka Maisha Yake Mapya Ndani ya Simba

Kocha huyo alitangazwa na uongozi wa Simba kuwa mkuu wa benchi la ufundi la  timu hiyo kwenye mechi za hivi karibuni.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa