Juma Mgunda aliekua kocha wa zamani wa Coastal Union ya Tanga ambae kwasasa anakaimu nafasi ya kocha mkuu wa klabu ya Simba amekanusha taarifa zilizozuka kua hana vyeti vya kuweza kuiongoza timu hiyo.

Baada ya kocha huyo kuchaguliwa kukaimu nafasi ya kocha mkuu wa klabu ya Simba siku ya jumatano usiku ziliibuka taarifa kua kocha huyo hana vigezo vya kukaa kwenye benchi la ufundi la klabu hiyo kwenye michuano ya kimataifa ambayo klabu hiyo inashiriki kwasasa.

MGUNDAKocha huyo ameweza kufunguka leo hii akiwa na timu  hiyo iliyopo nchini Malawi amesema akiposikia taarifa hizo hakupata wasiwasi kwani klabu ya Simba ni taasisi kubwa isingeweza kukurupuka mpaka kumchagua yeye kwani lazima ilifanya uchambuzi yakinifu kuweza kutambua kwamba ana vyeti au hana kama ambavyo inasemekana kwa baadhi ya watu.

Pia Mgunda ametupa lawama kwa baadhi ya waandishi wa habari kua hawataki kupata taarifa pande zote mbili akisema wakipata taarifa upande mmoja hawataki kusikiliza upande wa pili kwani habari hizo zilizushwa na baadhi ya wandishi wa habari na kushangazwa na kitendo cha kutomtafuta yeye ambaye ndio mhusika mkuu kuweza kupata ukweli wa mambo.

Aidha shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania(TFF) pia liliweza kutoa ufafanuzi juu ya hili ambalo lilikua linaendelea mitandaoni baada ya kutoa orodha ya majina ya makocha wenye vigezo na leseni za Caf na jina la kocha Juma Mgunda likiwemo kwenye orodha hiyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa