Vicente Del Bosque, nyakati fulani akiwa kocha wa Hispania katika ubora wake aliwahi kuulizwa swali kuhusu nafasi ya Isco Fransesco kikosini.
Del Bosque alijibu kwamba, Isco ni kati ya wale watoto wanaokera sana. Binafsi Isco alikuwa anamkera sana kwa alichokuwa anakifanya uwanjani.
Swali lililofuata ni kwanini Isco alikuwa anamkera wakati alikuwa katika kiwango bora sana. Kila kocha duniani angetamani awe na Isco katika timu yake.
Del Bosque alisema huo ubora wake ndio unamkera. Unajua kwanini?? Kwanza ulikuwa unamfanya akune kichwa juu ya nafasi yake kikosini. Pili ubora wa Isco ulikuwa unaitafutia dunia sababu ya kumlaumu Del Bosque.
Tayari alikuwa na rundo la viungo kisha alibakiwa na nafasi moja kati ya David Silva, Jesus Navas na Juan Mata. Ndipo jina la Isco likachomoza hapo katikati. Kama si kuitafutia dunia sababu ya kukulaumu ni nini?

Del Bosque alisema anachokifanya ni kukuna kichwa. Labda wakati anakuna kipara chake kinaweza kumpatia jibu. Nyakati hizo hata Carlo Ancelotti alikuwa hataki James Rodriguez atoke kwenye majeraha. Angemuambia nini wakati angekutana na Isco aliyewaka??
Ni hapo unapokitazama kikosi cha Yanga Afrika na kuvaa viatu vya kocha Nabi kisha unagundua hakuna anachoweza kufanya zaidi ya kukuna kichwa kwa sasa. Watoto wanakera sana!
Wakati unafikiria kumpatia nafasi Tonombe Mukoko atoke benchi mbele yako anakuja Zawadi Mauya kukuliza vipi mimi, si unaona ninachokifanya??
Unafikiria kutumia busara kumchezesha Bangala beki ya kati, unaona aibu kumtazama Bakari Mwamnyeto. Hapo bado una swali la kumjibu Sureboy kwa nafasi ya Fey Toto.
Unawaza kule kushoto Kibwana akirejea utamjibu nini ukizingatia Mustapha Yassin amecheza vema kipindi chote, achilia mbali David Bryson unayejua kwamba ukimpa nafasi atazidi kukutafutia sababu ya dunia kukulaumu.
Kwasasa Nabi anachoweza kufanya ni kukuna kichwa kama Del Bosque. Labda atapata majibu wakati akikuna kipara chake. Kwa sasa! Watoto wanazidi kuitafutia dunia sababu ya kumlaumu.
Vijana wanamuweka Professor Nabi katika wakati mgumu ambao kocha yoyote yule anaupenda. Ugumu wa kupanga kikosi kwasababu ya ubora ulionao!
Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.


