Kikosi bora cha PFA cha mwaka cha Premier League tayari kimetoka na licha ya kukosa ubingwa wa Ligi Kuu kwa pointi moja, Liverpool imeongoza kwa kutoa wachezaji waliojumuishwa kwenye Kikosi wakifuatiwa na City.
Liverpool wametoa wchezaji sita Manchester City watatu wakati Man United na Chelsea wametoa mchezaji moja moja.
Mlinda lango Alisson Becker, mabeki Trent Alexander-Arnold na Virgil van Dijk, kiungo Thiago Alcantara na washambuliaji Mohamed Salah na Sadio Mane wote walifanikiwa, wakati pia Salah akishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka.
Beki wa pembeni Joao Cancelo na viungo Bernardo Silva na Kevin De Bruyne walikamilisha wachezaji watatu wa City, kwa upande wa Chelsea walitoa mchezaji Antonio Rudiger wakati Christiano Ronaldo aliiwakilisha Manchester United.
Orodha kamili ya kikosi bora cha mwaka cha PFA Premier League 2022
GK: Alisson Becker (Liverpool)
RB: Trent Alexander-Arnold (Liverpool)
CB: Virgil van Dijk (Liverpool)
CB: Antonio Rudiger (Chelsea)
LB: Joao Cancelo (Manchester City)
CM: Bernardo Silva (Manchester City)
CM: Thiago Alcantara (Liverpool)
CM: Kevin De Bruyne (Manchester City)
RW: Mohamed Salah (Liverpool)
ST: Cristiano Ronaldo (Manchester United)
LW: Sadio Mane (Liverpool)
ALIYA’S WISHES
Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.