Mshambuliaji wa Manchester United Christiano Ronaldo alitikisa vichwa habari siku ya Jumamosi baada ya kuripotiwa kuomba kuondoka Old Trafford kwa madai ya kwamba anataka kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa kwa muda uliyo salia kwenye soka lake.

Mchezaji huyo wa miaka 37 alijiunga tena na Man United akitokea Juventus na amefanikiwa kufunga mabao 24 kwenye michuano yote na alitajwa mchezaji wa mwaka lakini jitihada zake binafsi zilishindwa kuipeleka Red Devils kwenye Champions League msimu huu.

United ilimaliza katika nafasi ya sita kwenye Premier League msimu uliyopita hali itakayowafanya washiriki michuano ya Europa League kitu kilichotabiriwa kuwa itakuwa ngumu kwa Ronaldo ambapo siku ya Jumamosi aliomba kuruhusiwa kuachana na klabu hiyo licha ya kusaliwa na mwaka mmoja na klabu hiyo ya jiji la Manchester.

Lakini ripoti za ndani zinadai kwamba Ronaldo hauzwi, wiki iliyopita kulikuwa na taarifa kwamba wakala wa Ronaldo alikutana na mmiliki mpya wa klabu ya Chelsea Todd Boehly hivyo huenda Ronaldo akajiunga na The Blues ambao watashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa