Kundi la utafiti la CIES Football Observatory limewataja wachezaji Kylian Mbappe, Vinicius Junior Erling Haaland na wengine ndiyo wenye thamani kubwa katika soka la dunia kwa sasa.

Mbappe ameongoza orodha ya wachezaji wenye thamani zaidi kuwa na msimu mzuri akiwa na Paris Saint-Germain, akiwa akiwa amehusika kwenye mabao 60 mabao 39, asisti 21 katika michezo 46 katika mashindano yote, anakadiriwa kuwa na thamani ya €205.6million (£175.7m).

Vinicius ameketi katika nafasi ya pili anakadiriwa kuwa na thamani ya €185.5m (£158.3m)  ameshinda LaLiga na Ligi ya Mabingwa mara mbili akiwa na Real Madrid.

Haaland ameshika nafasi ya tatu na hivi karibuni alihama kutoka Borussia Dortmund kwenda Manchester City kwa dau la €60m (£51m) baada ya kufunga mabao 86 katika mechi 89 alizocheza Ujerumani anadaiwa kuwa na thamani ya €152.9m (£130.4m) .

Utafiti wa CIES unatokana na hatua mbalimbali kama vile umri, thamani ya klabu, kiwango cha uchezaji wa wachezaji na mfumuko wa bei.

Orodha ya wachezaji kumi wenye thamani zaidi Dunia

1. Kylian Mbappe (PSG) – €205.6m (£175.7m)
2. Vinicius Junior (Real Madrid) – €185.5m (£158.3m)
3. Erling Haaland (Borussia Dortmund) – €152.9m (£130.4m)
4. Pedri (Barcelona) – €135.1m (£115.4m)
5. Jude Bellingham (Borussia Dortmund) – €133.7m (£114.2m)
6. Phil Foden (Man City) – €124.0m (£105.9m)
7. Frenkie de Jong (Barcelona) – €112.5m (£96.1m)
8. Luis Diaz (Liverpool) – €110.1m (£94.0m)
9. Ruben Dias (Man City) – €109.6m (£93.6m)
10. Ferran Torres (Barcelona) – €109.5m (£93.5m)


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa