Kocha wa muda wa klabu ya Manchester United Ralf Rangnick amesisitiza kuwa mashabiki wa timu hiyo wanahaki ya kupaza sauti kwa keeleza mawazo yao kufautia mgomo uliopangwa kwenye mchezo wa wikiendi.

Manchester United wanakutana na klabu ya Norwich City kwenye mchezo wa ligi kuu ya Uingereza siku ya jumamosi kwenye dimba la Old Trafford, na mashabiki wa wamepanga kuonyesha hisia zao za kutokuridhishwa na mmiliki wa klabu hiyo.

Ralf Rangnick
Ralf Rangnick

Kulikuwa na ulinzi mkali siku ya leo kwenye uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo Carrington training ground, baada ya mashabiki 30 kukusanyika wakiwa na mabango dhidi ya familia ya Glazer kutaka kuachia umiliki wa klabu hiyo.

Mashabiki wamekuwa wakiendelea kupaza sauti zao dhidi ya familia ya Glazer kuhusu deni kubwa ambalo wamelihamishia kwenye klabu hiyo, kutokuwepo na uwajiri mzuri na uwekezaji mbovu kwenye miundo mbinu ya klabu hiyo ambapo imewafanya kuwa nyuma ya vilabi shindani vya Liverpool na Man City.

Ralf Rangnick
Baadhi ya mashabiki wakiwa wameandamana kwenye lango la kuingilia uwanja wa mazoezini Carrington Park

Alipoulizwa kocha wa muda wa timu hiyo Ralf Rangnick kuhusu mgomo uliopangwa kwenye mchezo wa wikiendi dhidi ya Norwich.

“Tunajua kwamba mpira wa miguu ni mchezo wa hisia na shauku, nadhani sote  tunaweza kuwaelewa mshabiki wetu, kwenye nafasi tuliyopo sasa katita ligi lakini pia mchezo mbovu tuliounyesha dhidi ya Everton. 

“Lakini naamini mashabiki wetu ni miongoni kama sio mashabiki bora uingereza na kadri wanavyodhidi kupinga kwa utilivu na pia bado wanahamasika juha uwanjani, nafikili  wanahaki ya kueleza maoni yao. Naweza kuelewa kuwa wamevunjika sana moyo.” Alisema  Ralf Rangnick


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa