MABOSI wa Berkane FC ya nchini Morocco wamefunga safari kumfuata kiungo mchezeshaji, Feisal Salum ‘Fei Toto’ kwa ajili ya kuinasa saini yake ikiwa ni baada ya kukoshwa na uwezo wake ambao amekuwa akiuonyesha kila mara akiwa anaitumikia timu hiyo.

Kiungo huyo mara kadhaa amekuwa akiwaniwa vikali na baadhi ya klabu za nje ya nchi kwa ajili ya kumnasa tangu asajiliwe na klabu hiyo akitokea JKU ya kwao Zanzibar.

Azam FC nayo ilikuwa ikitajwa kuwepo katika mipango ya kumnasa kiungo huyo mara baada ya kumuwekea ofa nono ya Sh 350Mil sambamba na mshahara wa Sh 10Mil.

Taarifa zinadai kuwa , mabosi hao wa Berkane wametenga dau kubwa la fedha litakalomshawishi Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said ili akubali kumuachia kiungo huyo mwenye kiwango bora hivi sasa.

Fei Toto awindwa na Waarabu

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa ofa hiyo ambayo ni siri inatajwa kubwa ambayo ngumu kumzuia kujiunga na Berkane katika usajili huu wa Januari, mwakani.

Aliongeza kuwa kama Yanga itakubali kumuachia kiungo huyo, basi timu hiyo, itafaidika kutokana ukubwa wa dau la usajili licha ya Fei Toto kuwa na mkataba wa miaka miwili zaidi ndani ya Yanga.

“Berkane wameonekana kupania kumnasa Fei Toto ni baada kupanga kutangaza ofa kubwa kwa Yanga ambao wamekuwa wagumu kumuachia.

Fei Toto awindwa na Waarabu

“Hivyo upo uwezekano mkubwa wa Fei Toto kujiunga na Berkane katika usajili wa Januari. Kwani wametenga ofa hiyo nono ili wamshawishi Rais wa timu hiyo, Injinia Hersi na kama akikubaliana na ofa hiyo, basi atajiunga nayo,”alisema mtoa taarifa huyo.

Hersi alizungumzia hilo la kumuachia kiungo huyo hivi karibuni na kusema kuwa: “Tupo tayari kumuachia Fei Toto kuondoka Yanga lakini aende kucheza nje ya nchi na sio hapa ndani.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa