Klabu ya Tanzania Prisons imeahidiwa Kiasi cha Shilingi milioni 10 kama wataifunga Azam Fc leo katika uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya na kama wakipata sare milioni 5.
Ahadi hiyo imetolewa na wadhamini wao ambao ni kampuni ya usafirishaji baharini Silent Ocean Ltd. Kwenye mechi ya Simba SC waliahidiwa milioni 20.
Tanzania Prisons wanacheza mchezo wao mwingine wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wao uliopita wa ligi kuu dhidi ya Simba kwa bao moja, goli likifungwa na Jonas Mkude dakika za lala salama.