Simone Kuhusu Lukaku

Kocha mkuu wa Intermilan Simone Inzaghi amekiri kuwa mara zote anahisi hatarini na anathibitisha kuwa mshambuliaji wake Romelu Lukaku anahitaji muda zaidi kupona jeraha lake.

 

Simone Kuhusu Lukaku

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji alitarajiwa kurejea uwanjani dhidi ya Roma kesho, lakini Inzaghi amefichua kwamba atalazimika kucheza mchezo huo  bila mchezaji huyo wa Chelsea aliye kwa mkopo dhidi ya kikosi cha José Mourinho.

“Kulikuwa na kuchelewa kidogo. Mwezi umepita, lakini atahitaji muda zaidi, “aliwambia Wanahabari, kama ilivyonukuliwa na Tuttomercatoweb.

Lukaku sio pekee atakayekosekana kwenye mechi dhidi ya Roma, kwani mchezaji mwingine Marcelo Brozovic atakuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya mwezi mmoja kufuatia jeraha alilopata akiwa na timu ya taifa ya Croatia.

 

Simone Kuhusu Lukaku

Simone Inzaghi na wachezaji wake wamekuwa katika hali ngumu baada ya kuwa na mwendelezo mbaya katika Serie A hukunafasi yao ya kuwania taji la ligi hiyo hapo Italia huku wapinzani wao wakiwa na mwendelezo wa kuvutia.

Acha ujumbe