Nyota wa Yanga Wampa Mbinu ya Kibabe Nabi

Ikiwa kesho kutwa Jumatano ndiyo inakwenda kujulikana hatma ya Yanga kwenye mashindano ya kimataifa watakaposhuka dimbani kucheza na Club Africain, mastaa wa zamani wa klabu hiyo wameibuka na kumpa kocha Mohamed Nabi mbinu ya ushindi.

Mastaa hao ni Mohamed Hussein (Mmachinga) ambaye ni kocha msaidizi wa Yanga Princess na beki wa zamani wa timu hiyo Bakari Malima (Jembe Ulaya) ambao kwa pamoja walisema Nabi akitakiwa kufanikiwa ni kupata mabao ya mapema.

Mmachinga alisema: “Mchezo bado upo wazi na Yanga tuna nafasi kubwa ya kusonga mbele. Kubwa kocha Nabi anatakiwa asisitize wachezaji wake kwenye kupata mabao ya mapema na kuwa na umakini kwenye kujilinda.”

Kwa upande wa Malima yeye alisema: “Nabi hana haja ya kuwaambia wachezaji wake wajilinde, waende wakacheze na kushambulia, jambo kubwa wakawe makini kwenye kila tukio kwa sababu wale waarabu ni wajanja sana.

“Ushindi wa bila kufungana hapa nyumbani kwetu sisi ni faida kwa sababu tunatakiwa kupata bao angalau moja la haraka na kucheza kwa tahadhari kubwa. Naamini Nabi analijua hili na hatotuangusha,”

Yanga kesho wanatakiwa kupata ushindi au sare ya mabao ambayo inaweza kuwapa nafasi ya kuvuka na Kwenda hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho Afrika.

Acha ujumbe