Timu ya Kiwalani United imeibuka mshindi wa fainali za Meridianbet Soka Bonanza zilizofanyika leo kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Kiwalani, kwa mikwaju ya penati 5-4 ambapo mchezo ulienda mpaka kipindi cha pili bila mshindi kupatikana, ikabidi mshindi apatikane kwa mikwaju ya penati.

Mshindi wa Kwanza alipata zawadi ya Seti ya Jezi kamili 1, mipira miwili, soksi pea 3, glovu 1 na kitambaa cha unahodha. Na mshindi wa pili alipata zawadi ya Jezi Seti moja kamili, mipira miwili, soksi pea moja, glovu na kitambaa cha unahodha.meridiannetMchezo wa kwanza ulichezwa kati ya Ajax FC dhidi ya Kiwalani United mchezo uliojaa ufundi mkubwa na wachezaji wengi wenye vipaji, lakini mpaka dakika 90 hakupatikana mbabe.

Baada ya Dakika 90, ilibidi kanuni zifuatwe kwa kutumia mikwaju ya penati ndipo mshindi aliyeenda kucheza fainali alipatikana, Ajax FC walitolewa kwa mikwaju ya penati, 5-3.

Mechi ya pili ilikuwa ni kati ya Kiwalani Boys dhidi ya Kigilagila FC ambao kwa asilimia kubwa ilikuwa na vijana wengi wanaochipukia, wakati Kiwalani Boys wakitumia udhaifu wa Kigilagila FC na kuwafunga magoli 2-0 na hivyo kuwalazimisha kucheza mechi ya mshindi wa tatu.meridianbetMshindi wa 3, alikuwa ni timu ya Ajax FC ambapo walipata Zawadi ya seti moja kamili ya jezi, mpira mmoja, soksi 1, glovu ya mlinda mlango 1 na kitambaa cha unahodha kimoja.

Hakika Meridianbet Soka Bonanza lilinoga na kila aliyehudhuria hakujutia wikiendi yake, kwani mbali na zawadi kwa washindi hata mashabiki walipata burudani ya kutosha.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa