Serena Anaidai Shkamoo ya Dada Yake, Venus!

Ama kwa hakika kwenye nia pana njia, ndiyo maneno ya Wahenga yenye maana kuwa na nia ni nguzo muhimu katika kuyafikia malengo yako. Bwana Richard William, baba wa wachezaji maarufu na wenye ubora wa hali ya juu wa mchezo wa tenisi, Venus na Serena alijipinda na kuandaa mipango mahusus ambayo matunda yake tunayaona leo hii. Mzee Richard pamoja na mkewe Oracene Price waliwapata watoto hao Venus, Juni 17, 1980 na Serena Septemba 27, 1981 ambapo walihusika kwa kiwango kikubwa katika kuwapika au kuwaandaa wachezaji hao maarufu.

Mzee Richard alitokea sana kuupenda mchezo wa tenisi (mchezo ambao kati kuna wavu unaoishia magotini, wachezaji hukaa pande mbili wakipigiana mpira mdogo au kitenesi kuvuka ule wavu hadi ng’ambo ya mpinzani). Hivyo alianda mikakati imara ya kuzalisha wachezaji haswa akiwalenga wanaye hao wa kike. Mzee huyo aliandaa kurasa 78 zinazohusu namna ya kuwa mchezaji bora wa tenisi na akalazimika kuwafunza wanaye tenisi walipofikisha miaka 4 na nusu tu. Mkewe Price aliwafunza namna ya kukipiga kitenesi na yeye aliwafunza zaidi nidhamu ya mchezo.

Miongoni mwa mambo aliyowafunza ni vitu muhimu vitano vya kuzingatia ni Mungu, familia, elimu, biashara na mwisho, tenisi. Pia, aliwafunza umoja na kujitambua mwenyewe. Fortune favors all the brave wasemavyo Wazungu kuwa yule mwenye akili au nguvu mara nyingi huwa ndiye mwenye bahati, basi hilo pia lilitokea kwa wadada hawa.

Kwanza mambo yalianza kumuendea vizuri Venus ambaye ndiye aliyekuwa mkubwa. Venus alifika hatua ya kuwa namba moja duniani kwa wanawake mwaka 2002 na akadumu kwa wiki 11. Akiwa peke yake Venus alifanikiwa kushinda vikombe 49, pia alishinda medali 4 za dhahabu za Olimpiki na moja ya silva ikumbukwe kuwa tatu kati ya hizo alishinda akiwa na mdogo wake. Akiwa kama timu au watu wawili Venus alishinda mataji 21 mengi ya hayo akiwa na mdogo wake. Ingawaje alishinda makombe makubwa kama U.S, French, Wimbledon na Australia Open lakini kikwazo kikubwa alikuwa ni mdogo wake Serena. Kwani walipokutana mara nyingi Serena aliibuka mbabe. Hapa Serena alimdhirishia dada’ke kuwa umenizidi umri tu ila siyo uwanjani haaaahaaahaa yaani nitakupa shkamoo asubuhi ila nawe utanipa shikamoo uwanjani.

Kwa upande wa Serena yeye alisubiri kwanza dada yake aanze kwanza ndipo naye akafuata. Mwanzoni hakuwa imara sana kwani walipokutana na dada yake alichezea kichapo tu. Wadada hawa walikutana kwa mara ya kwanza 1998 kwenye Australian Open na Serena akakiri kuwa sijakuwa vizuri ndiyo maana umeshinda. Baada ya hapo moto ukawaka kweli kweli maana kuanzia Julai 2002 Serena akawa naamba moja tena kwa wiki 316 na zaidi, takwimu hizo zilitolewa na Women’s Tennis Association.

Kiujumla Serena alikuwa na mafanikio zaidi kuliko dada yake kwani alishinda mataji 73 akiwa peke yake na 23 akiwa kama timu ya watu wawili. Pia, alishinda medali 4 za dhahabu za Olimpiki tatu kati ya hizo akiwa na dada yake. Ama kwa hakika Richard na Oracene waliaanda washindani waliokuwa wanachuana wenyewe duniani.

Wakiwa pamoja Venus na Serena au Williams family walifanya makubwa duniani. Walichukua medali tatu za Olimpiki tena medali za dhahabu. Pia, walichukua mataji ya Grand Slam kumi na nne wakiwa pamoja ama kwa hakika walifanya maajabu. Pia, mnamo mwaka 2002 Venus alikuwa namba moja na Serena namba mbili kwa ubora duniani. Mwaka elfu mbili na kumi mambo yalikuwa hivyo hivyo tena ila safari hii mdogo (Serena) alikuwa namba 1 na Venus dada mtu namba 2. Raha iliyoje baba na mama kuwatengeneza mashujaa kupitia watoto wao. Uzuri ni kuwa waliwashinda wenzao kutokana na kufanya mazoezi pamoja yaani walikuwa wanashinda washindi watupu mazoezini na kupambana na watu dhaifu kwenye mechi zenyewe haahahaahaa.

Dunia haishi vituko ndiyo mahala pekee kwa kutokea vituko ni duniani basi mzee Richard alikuwa kituko kweli kweli. Mzee Richard hakujulikana kuwa anampenda yupi kati ya watoto wake, hivyo ikitokea wanakutana basi jua kuwa atajificha asione. Pia, hatopata matokeo na hataki watu wampe matokeo kiufupi alikuwa katika hali ngumu. Mzee huyo alikuwa anawaza ni namna gani mtoto wake aliyeshindwa anayapokea matokeo hayo. Kweli dunia sinia pakua unachokiweza, ndiyo unasubiri nini kupakua. Mzee Richard anakula kupitia wanawe wenyewe haaaswaaa maana kuku kwa mrija yeye ndiye kocha ambaye anatumbua hela za wanawe.

3 Komentara

    Duuh serena nomaa

    Jibu

    Nimependa sana history yao amahakika kutangulia mbele si kufika wa kwanza pongezi kwa Serena

    Jibu

    Kweli kutangulia siho kufika Dada kanza mwisho wasiku mdogo mtu ujakumpikuwa Dada mkubwa kweli Anastairi pongez Serena yeye nafamily yake mzee Richard alipanga family yake inavyo stairi pongezi kwao

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.