Kocha wa Arsenal Mikel Arteta amefurahi kuirudisha timu hiyo mahala inapo pahusu akiwa na kikosi kichanga baada ya miaka miwili akiwa kama meneja.
Kocha huyo ambaye aliwahi kuichezea klabu hiyo miaka ya nyuma alichaguliwa kuinoa Arsenal mwaka 2019 mwezi Disemba huku akiwa amefanikiwa kutwaa taji la FA na Ngao ya Jamii kwa mwaka wake wa kwanza.
Lakini Arteta bado anadeni la kutoipeleka Arsenal kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa tangia akabidhiwe mikoba ya kuifundisha timu hiyo.
“Sasa ni awamu mpya ambapo tunaanza kuijenga upya timu, tunachukua mwelekeo wa wazi kabisa wa jinsi tunavyotaka kusonga mbele na klabu, uhusiano wa kweli kati ya timu na mashabiki, umiliki na bodi na nadhani sasa ni msisimko, “Arteta aliambia tovuti rasmi ya Arsenal.
“Furaha ya kuendeleza mradi huu mbele, kuendelea kufanya kazi na kikosi hiki changa kweli, lakini tayari kushindana, ili kuwa bora na kurudisha klabu mahali inapostahili.”
Nani hapendi kuwa bingwa na kujishindia mkwanja wa kusahato kuelekea katika sikukuu wiki hii. Mchezo wa Ocean Call kutoka kasino maridhawa za meridianbettz unakupa kila sababu ya kuifanya siku kuu yako kuwa ya kuvutia zaidi.