Mchezaji wa klabu ya Fc Barcelona Pierre Emerick Aubameyang hatma yake haijajulikana ndani ya klabu hiyo. Nyota huyo raia wa Gabon ambae alijiunga na klabu hiyo akitokea klabu ya Arsenal ya nchini Uingereza katika dirisha dogo mwezi Januari.
Mchezaji wa klabu ya Fc Barcelona Pierre Emerick Aubameyang hatma yake haijajulikana ndani ya klabu hiyo. Nyota huyo raia wa Gabon ambae alijiunga na klabu hiyo akitokea klabu ya Arsenal ya nchini Uingereza katika dirisha dogo mwezi Januari.

Klabu ya Fc Barcelona inapitia matatizo ya kiuchumi kwa muda sasa, hivyo Barca wanalazimika kuwauza baadhi ya nyota wake ili kutengeneza usawa wa kifedha. Ukiachana na tatizo la fedha ndani ya Barca.
Pia ujio wa aliekua nyota wa klabu ya Fc Bayern Robert Lewandowski ndani ya Barcelona ambae anakuja kucheza nafasi anayocheza Aubameyang kuna kila dalili Auba kukosa nafasi ndani ya Barca, kitu ambacho kinamfanya kufikiria kutafuta changamoto nje ya Barcelona.
Nyota huyo wa zamani wa vilabu vya Dortmund na Arsenal inaelezwa anatizamia kwenda klabu inayoshiriki ligi ya mabingwa barani ulaya. Wakati huoho klabu ya Chelsea inaiwinda saini ya staa huyo kwa karibu sana ikumbukwe klabu ya Chelsea imekua ikipitia changamoto ya kukosa mshambuliaji mwenye makali kwa muda mrefu.
Pia Chelsea dirisha hili wameuza washambuliaji wao wawili ambao ni Romelu Lukaku pamoja na Timo Werner ambao wote wamekwenda kwa mkopo kwenye team zao za zamani.
Chelsea wanataka kuongeza nguvu kwenye safu yao ya ushambuliaji baada ya kumsajili Raheem Sterling kutoka klabu ya Manchester City huku Pierre Emerick Aubameyang akiwa kwenye orodha ya wanaotakiwa katika nafasi hiyo na wakimtizama kama chaguo sahihi kwao.

